Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 29, 2024 Local time: 02:03

Trump ahojiwa chini ya nusu saa


Mahojiano ya lazima ya Rais mstaafu wa Marekani, Donald Trump, ya Jumatatu yalimalizika chini ya nusu saa ya maswali na majibu ya kawaida, mtu anayefahamu suala hilo ameliambia shirika la habari la Associated Press.

Mtu huyo hajaidhinishwa kuzungumzia shauri hilo hadharani na amezungumza kwa masharti ya kutotambulishwa.

Rais huyo wa zamani aliulizwa maswali na afisa wa uangalizi wa jiji la New York kwa ripoti ambayo itakusanywa na kuwasilishwa kwa hakimu wa mahakama Juan M. Merchan kabla ya hukumu yake Julai 11 katika kesi yake ya jinai ya kumnyamazisha mtu.

Merchan anaweza kutumia ripoti hiyo kusaidia kuamua adhabu ya Trump kufuatia kutiwa hatiani Mei 30 kwa kughushi rekodi za biashara ili kuficha kashfa ya ngono.

Hakimu anaweza kutoa adhabu mbalimbali kwa Trump, kuanzia muda wa uangalizi, kutoa huduma kwa jamii, mpaka kifungo cha miaka minne gerezani.

Forum

XS
SM
MD
LG