Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 12:51

Trump asema watu wanapiga kura kinyume cha sheria


Rais wa zamani Donald Trump
Rais wa zamani Donald Trump

Rais wa zamani Donald Trump, mgombea urais mtarajiwa wa chama cha Republican, anasema watu wanapiga kura kinyume cha sheria katika uchaguzi wa Marekani, ikiwa ni pamoja na wahamiaji.

Mji mmoja huko California umeweka kanuni za Kitambulisho cha mpiga kura hatua ambayo inakiuka sheria za upigaji kura za jimbo. Genia Dulot anaripoti na Khadija Riyami anaisoma ripoti kamili.

Pwani ya kupendeza ya Huntington inajulikana kama “Surf City, USA.” Lakini umaarufu wake wa kisiasa katika uchaguzi wa mwaka huu ni kuhusu sheria ya serikali za mitaa inayotaka picha kwenye kitambulisho kabla yamtu kupiga kura. Meya Gracey Van Der Mark anasema inaonyesha wasi wasi wa raia kuhusu uadilifu katika uchaguzi.

Gracey Van Der Mark, Meya wa Huntington Beach anasema: “Huwezi hata kwenda kumuona daktari wako bila ya kitambulisho, lakini jambo muhimu katika nchi yetu – mfumo wetu wa uchaguzi – kwasababu kila kitu tunachokifanya kinawahusu wanasiasa ambao tunawaweka madarakani. Maisha yetu yanaongozwa na yule ambaye tunamuweka madarakani, na wanapoanza kupitisha sheria, kwahiyo tunataka kuhakikisha kuwa uadilifu katika uchaguzi wetu unalindwa.”

Wasiokuwa Raia Kupiga Kura

Wasiokuwa raia kupiga kura ni suala la kisiasa katika kampeni ya urais hivi sasa. Akiwa huko Arizona wiki iliyopita, Donald Trump alimshutumu Joe Biden kwa kuwaruhusu wahamiaji kuvuka mpaka wa Mexico kinyume cha sheria na kumpigia kura katika uchaguzi wa Novemba.

Donald Trump, Mgombea Urais wa Republican anasema: “Mtu aje atueleze kwanini wanataka hili litokee. Nadhani kwa hakika ni kupata kura.”

Hakuna ushahidi kwamba wasiokuwa raia wanapiga kura kwa idadi kubwa katika chaguzi za Marekani.

Wapiga kura wengi Marekani wanathibitisha habari zinazowahusu wanapofika kupiga kura, lakini hawahitajiki kuonyesha kitambulisho.

Mwakilishi wa Huntington Beach Dan Kalmick anapinga kuwa hatua ya kitambilisho kwa mpiga kura na kusema inaonyesha kuelemea kwa mji huo katika mrengo wa kiconservative zaidi.

Dan Kalmick, Mwakilishi wa Huntington Beach anasema: "Kitambulisho cha mpiga ni kwa ajili ya yule anayefika binafsi kupiga kura, lakini ni asilimia 15 tu ya walifika binafsi kupiga kura katika uchaguzi uliopita. Wanajaribu kusuluhisha tatizo gani? Tunajaribu kusuluhisha kwa ajili ya maelfu ya watu ambao watakwenda kupiga kura binafsi? Kwa mara nyingine inathibitisha hilo ni suala la kisiasa. Kwa hakika hakuna tatizo ambalo tunajaribu kulisuluhisha.”

California Inasheria Zake za Uchaguzi

California ina sheria zake za uchaguzi, na jimbo linaishtaki Huntington Beach

Juu ya hatua ya Mwanasheria Mkuu Rob Bonta inawaathiri zaidi “wapiga kura wa kipato cha chini,

Wapiga kura wasio wazungu, wapiga kura vijana au wazee, na watu wenye ulemavu.”

Charlie Zablah ni mhamiaji ambaye anamiliki mhagawa wa Mediterranean. Anasema hatua ya kitambulisho cha mpiga kura haibagui.

Charlie Zablah, Mmiliki wa “Charlie’s Gyros” anasema: “Kwasababu tu wewe ni maskini, haina maana huna leseni za udereva, au huwezi kuwa na leseni ya kuendesha gari.”

UNIDAD

Kundi lilisilo la kiserikali la Oak View Com UNIDAD linafanya kazi “kuondoa mwanya wa kijamii, kitamaduni, afya na kiuchumi” huko Huntington Beach.

Mwanzilishi mwenza Oscar Rodriguez

… anasema sheria itakandamiza idadi ya wapiga wa kipato cha chini kujitokeza katika ujirani wao.

Oscar Rodriguez, Mwanzilishi Mwenza, Oak View Com UNIDAD anasema:

“Mwawachanganya watu na hivyo, wakati tayari kuna idadi ndogo ya wapiga kura inayojitokeza, huenda ni kwasababu ya huduma ya watoto, kuwa na kazi kadhaa, kwasababu hawauamini mfumo. Halafu unaongezea jambo jingine kitambulisho cha mpiga kura, halafu mambo kama hayo yanawachanganya watu, na huenda ikawafanya wasifike katika vituo na kupiga kura.”

Wakuu wa mji wanasema tayari wako tayari kupigania juu ya kitumbulishi cha mpiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa. Changamoto hizo za kisheria zitaichukua kesi hadi upigaji kura wa mwezi Novemba, wakati sheria za jimbo za upigaji kura zitaendelea kuwepo huko.

Forum

XS
SM
MD
LG