Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 08, 2024 Local time: 10:04

Balozi wa Marekani amjibu Rais Samia


Balozi wa Marekani nchini Tanzania Michael Battle.
Balozi wa Marekani nchini Tanzania Michael Battle.

Balozi wa Marekani nchini Tanzania amesisitiza hataacha kuzungumzia maswala ya demokrasia na haki za binadamu kinyume na alivyoagiza rais Samia Suluhu Hassan.

Balozi wa Marekani nchini Tanzania Michael Battle amesisitiza kwamba Marekani haitaacha kukosoa ukiukwaji wa haki za binadamu na kuminywa kwa demokrasia endapo utatokea katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki, akisisitiza kwamba ni muhimu kwa utawala kuchukua kila juhudi na kuhakikisha kwamba raia wa Tanzania wanafurahia demokrasia na kuishi katika misingi ya haki zao.

Battle amesema kwamba kama mshirika wa Tanzania siku zote Marekani haitanyamaza pale kuna uvunjaji wa sheria, demokrasia na haki za kibinadamu.

Balozi Michael Battle amesema ataendelea kuzungumza kwa uwazi kabisa na kwa ukweli kuhusu mambo yanayoihusu Tanzania.

Amesisitiza kwamba hawatakoma kufuatilia maswala ya demokrasia na haki za binadamu na kwamba hilo ni jukumu muhimu kabisa kwa maslahi na heshima ya ubinadamu.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan Picha na HANNAH MCKAY / POOL / AFP.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan Picha na HANNAH MCKAY / POOL / AFP.

Matamshi yake yanakuja siku chache baada ya rais Samia Suluhu Hassan kuwataka mabalozi wa mataifa ya nje walioko nchini Tanzania kuacha kuzungumzia mambo ya ndani ya Tanzania, akitishia kuzungumza moja kwa moja na marais wa nchi za magharibi kuhusu mienendo ya mabalozi wao walio Tanzania.

Mabalozi wa Marekani, Uingereza, Umoja wa Ulaya, Canada miongoni mwa nchi nyingine za Magharibi walitoa taarifa iliyotaka uchunguzi huru ufanywe kuhusiana na mauaji na utekaji nyara wa wanasiasa wa upinzani.

Mabalozi hao walitoa taarifa kufuatia kuuawa kwa mwanasiasa wa chama kikuu cha upinzani CHADEMA, Mohamed Ali Kibao. Kuna ripoti pia za wanasiasa kadhaa wa upinzani na wanaharakati kupotea.

Forum

XS
SM
MD
LG