Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 03, 2025 Local time: 06:31

Rais Samia afanya mabadiliko Baraza la Mawaziri, Makamba na Nape watenguliwa

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan. Picha na Tchandrou Nitanga / AFP.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan. Picha na Tchandrou Nitanga / AFP.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa mawaziri wawili akiwemo Januari Makamba (waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki) katika mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri, ofisi yake ilisema.

Pia ametengua uteuzi wa waziri Nape Nnauye ( waziri wa habari, mawasiliano na teknolojia ya habari.

Mbali na hao, Rais Samia ametengua uteuzi wa Stephen Byabato aliyekuwa naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Rais amemteua pia Ridhiwani Kikwete kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu).

Wengine walioteuliwa na Rais Samia ni Jerry Silaa anakuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari. Kabla ya uteuzi huo alikuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Balozi Mahmoud Thabit Kombo ameteuliwa kuwa Mbunge na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kabla ya uteuzi huo alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia.

Forum

XS
SM
MD
LG