Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za mitaa nchini Tanzania, zimefunguliwa rasmi Novemba 20, huku kukiwa na sintofahamu kwa baadhi ya wagombea kutoka vyama vya upinzani ambao wameenguliwa, wakiwemo wale wa vyama cha CHADEMA na ACT Wazalendo.
Zaidi ya vijana 500 kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika Jumatatu wamekutana Jijini Arusha ,Tanzania kujadili namna watakavyoweza kupata fursa na haki ya kumiliki ardhi katika nchi zao, na kuitumia kujikwamua kwenye umaskini.
Watu wasiojulikana walimteka nyara, kumpiga na kumjeruhi vibaya afisa mwandamizi wa chama cha upinzani nchini Tanzania Chadema
Wakati Dunia ikiadhimisha siku ya Chakula wakulima nchini Tanzania wametakiwa kuendelea kulinda vyakula vya asili ambavyo vipo hatarini kutoweka kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.
Watetezi wa haki za watoto wa kike nchini Tanzania wameitaka serikali kubadilisha kipengele cha sheria ya ndoa ya kinachotoa ruhusa kwa mtoto wa kike kuolewa akiwa chini ya umri wa miaka 18.
Tanzania itaendelea kuunga mkono juhudi za kurejesha hali ya amani na usalama zinazoendelea kufanywa sehemu mbalimbali barani Afrika ikiwemo Ukanda wa Afrika Magharibi, Pembe ya Afrika na Sudan Kusini.
Wakati Dunia ikiadhimisha siku ya utalii Duniani vijana nchini Tanzania wametakiwa kuwa wabunifu ili kuendana na ukuaji wa sekta ya utalii na kuwawezesha kujipatia ajira kupitia ubunifu unaoendana na mahitaji ya utalii nchini.
Viongozi wakuu wa upinzani nchini Tanzania waliachiliwa Jumatatu jioni, chama chao kimesema, baada ya kushikiliwa na polisi ambao walizuia maandamano yaliyokuwa yamepangwa jijini Dar Es Salaam katika hatua ya hivi karibuni ya kuwanyamanzisha wapinzani.
Polisi nchini Tanzania Jumatatu imewakamata viongozi wawili wa upinzani, chama chao na polisi wamesema, kwa azma ya kuzuia maandamano ya dhidi ya serikali yaliyopangwa kufanyika katika mji mkuu wa kibiashara Dar es salaam.
Mkuu wa jeshi la Uganda, ambaye ni mtoto wa kiume wa rais Yoweri Museveni, Generali Muhoozi Kainerugaba, amesema kwamba hakuna rais atakayeongoza Uganda na kwamba hilo ni jukumu la wanajeshi au polisi.
Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kimetoa ripoti iliyoonyesha mafanikio katika kuimarisha demokrasia nchini huku kukiwa na ushiriki mdogo wa vijana, wanawake, na watu wenye ulemavu katika nafasi za uongozi.
Balozi wa Marekani nchini Tanzania amesisitiza hataacha kuzungumzia maswala ya demokrasia na haki za binadamu kinyume na alivyoagiza rais Samia Suluhu Hassan.
Pandisha zaidi