Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na JWTZ, inaeleza wanajeshi hao wamefariki dunia kutokana na mfululizo wa mashambulizi yaliofanywa na wapiganaji wa kundi la M23, kati ya Januari 24 na 28 katika maeneo ya Sake na Goma.
Taarifa taarifa imeongezea kueleza kuwa wanajeshi wengine wanne walijeruhiwa wakati wa mashambulizi na wanapatiwa matibabu katika mji wa Goma, ambao tayari unashikiliwa na waasi wa M23 wanaodaiwa kusaidiwa na Rwanda.
Mkurugenzi wa habari na uhusiano jeshi la ulinzi wa wananchi wa Tanzania, Kanali Gaudentius Gervas Ilonda, amesema taratibu za kusafirisha miili ya wanajeshi hao pamoja na majeruhi zinaendelea kupitia sekretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, SADC.
Kanali Gaudentius, ameongeza kusema vikundi vya wanajeshi wa Tanzania vilivyopo, DRC, vipo salama, imara na vinaendelea kutekeleza majukumu yake kwa maelekezo ya uongozi wa SADC.
Wanajeshi wa Tanzania, ni miongoni mwa wale kikosi cha kulinda amani kutoka SADC, ambacho kilipelekwa kusaidia nchi mwanachama DRC, pamoja na mataifa mengine ya Kusini mwa Afrika.
Afrika Kusini yenyewe ilipoteza wanajeshi 13 ambao walikuwa kwenye kikosi hicho. Taarifa ya JWTZ inafanya idadi ya wanajeshi wa SADC waliouwawa DRC, kuongezeka.
Forum