Freeman Mbowe aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha Chadema kwa miongo miwili amempongeza mrithi wake Tundu Lissu mara baada yakutangazwa mshindi.
Katika akaunti yake kwenye mtandao wa X bwana Mbowe aliandika “ nampongeza mweshimiwa Tundu Lissu na wenzake kwa kuaminiwa na wajibu wa kukiongoza chama”.
Mabadiliko hayo yanakuja wakati ambapo kuna ukandamizaji mkubwa kwa upinzani katika taifa hilo la Afrika Mashariki pamoja na migawanyiko ya ndani katika chama cha Chadema ambacho wachambuzi wanasema inaweza kudhoofisha nafasi yake katika uchaguzi mkuu.
Mkutano mkuu wa chama ambao unamchagua mwenyekiti kila mwaka ulianza mapema Jumanne na kuendelea hadi usiku.
Lissu aliyekuwa mgombea wa urais wa Chadema katika uchaguzi uliopita wa mwaka 2020 alimshutumu Mbowe kwa kukaa madarakani kwa muda mrefu na kuahidi mageuzi ndani ya chama.
Forum