Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Novemba 21, 2024 Local time: 21:27

Viongozi wa Chadema waachiliwa kwa dhamana


Mwenyekiti wa Chama kikuu cha upinzani CHADEMA Freeman Mbowe alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kukamatwa . Picha na VOA
Mwenyekiti wa Chama kikuu cha upinzani CHADEMA Freeman Mbowe alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kukamatwa . Picha na VOA

Viongozi wakuu wa upinzani nchini Tanzania waliachiliwa Jumatatu jioni, chama chao kimesema, baada ya kushikiliwa na polisi ambao walizuia maandamano yaliyokuwa yamepangwa jijini Dar Es Salaam katika hatua ya hivi karibuni ya kuwanyamanzisha wapinzani.

Licha ya marufuku rasmi, Chadema kiliapa kusonga mbele na maandamano ya kupinga kile kinadai ni utekaji nyara na mauaji ya wanachama wake yanayofanywa na maafisa wa usalama.

Polisi wa kuzima ghasia walikuwa wamejipanga jijini kote wakiwa na mabomu ya kurusha maji ya kuwasha ili kuzuia mikusanyiko, na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Makamu wake Tundu Lissu walikamatwa haraka pamoja na wengine kadhaa.

Baadaye Jumatatu jioni, chama hicho kiliandika kwenye mtandao wa X kwamba Mbowe na Lissu, pamoja na afisa mwingine mkuu wa chama, waliachiliwa kwa dhamana.

Hata hivyo, Mbowe “aliamua kubaki katika kituo cha polisi hadi wanachama na wafuasi wengine waliokamatwa wapewe dhamana,” Chadema kimesema.

Chama hicho kinaituhumu serikali ya Rais Samia Suluhu kuirejesha nchi kwenye mbinu za ukandamizaji za mtangulizi wake, hayati John Magufuli.

Forum

XS
SM
MD
LG