Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 02, 2025 Local time: 23:38

Jumuia ya Afrika Mashariki yaiomba DRC kuzungumza na waasi wa M23


Rais wa Kenya William Ruto akizungumza wakati wa uzinduzi wa majadiliano ya kutafuta amani DRC, Nairobi, Novemba 28, 2022.Picha ya AP
Rais wa Kenya William Ruto akizungumza wakati wa uzinduzi wa majadiliano ya kutafuta amani DRC, Nairobi, Novemba 28, 2022.Picha ya AP

Jumuia ya Afrika Mashariki Jumatano imeitaka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuzungumza na “wadau wote”, wakiwemo wapiganaji wanaoungwa mkono na Rwanda, ili kumaliza mapigano katika eneo la mashariki mwa nchi.

Katika mkutano kwa njia ya video, viongozi wa nchi za jumuia hiyo wametoa wito wa “kumaliza mizozo kwa njia ya amani, na kuiomba kwa dhati serikali ya DRC kuanzisha mazungumzo ya moja kwa moja na wadau wote, ikiwemo kundi la M23 na makundi mengine yenye silaha ambayo yana malalamiko,” ilisema taarifa ya viongozi hao.

Forum

XS
SM
MD
LG