Rais wa zamani wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi, amefariki leo Alhamisi akiwa na umri wa miaka 98, vyanzo vya habari nchini Tanzania vimeeleza.
Mwili wa raia wa Tanzania umepatikana ukielea katika Mto Miami Marekani Jumanne asubuhi na idara husika zikithibitisha kuwa mwili huo ni wa mtu aliyeanguka kutoka katika mashua mwishoni mwa juma.
Wahifadhi wa mazingira na wanyama pori wa Afrika Kusini wameonya Jumanne kwamba kuna ongezeko kubwa la ujangili wa wanyama pori, wakiwemo wanyama takriban 500 wameuawa mwaka jana.
Baadhi ya wachumi na wasomi nchini Tanzania weitaka serikali kuhakikisha mradi wa reli ya umeme SGR unaleta manufaa kwa wananchi wa matabaka yote kwa kutoa huduma zenye bei nafuu huku wakishauri mradi huo ujikite katika usafirishaji wa mizigo ili kuhakikisha unarudisha uwekezaji uliofanyika.
Kauli mbiu ya Siku ya Radio Duniani mwaka 2024 inaangazia kwa upana mafanikio ya radio yaliyofikiwa siku za nyuma, uhalisia wake hivi sasa na maendeleo ya mustakbali wake.
Kukosekana kwa uhuru wa vyombo vya habari kutoa baadhi ya habari pamoja na kuwepo kwa idadi kubwa ya kodi na tozo ni miongoni mwa changamoto zinazosababisha ugumu katika uendeshaji wa vyombo vya habari nchini Tanzania .