Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:02

Burundi wapoteza ushiriki wa BAL kwa kukataa kuvaa jezi yenye nembo ya Visit Rwanda


Amadou Gallo Fall (Seydina Aba Gueye / VOA)
Amadou Gallo Fall (Seydina Aba Gueye / VOA)

Wawakilishi wa Burundi katika michuano ya  mwaka huu ya Ligi ya Mpira wa Kikapu Afrika- BAL katika  mashindano yanayofadhiliwa na  Chama cha mpira wa  Kikapu NBA tawi la Afrika Jumatatu walipoteza ushiriki wao baada ya kukataa kuvaa jezi yenye nembo ya Visit Rwanda.

Klabu ya Mpira wa Kikapu ya Dynamo, mabingwa wa Burundi wanaoshiriki kwa mara ya kwanza kwenye Ligi hiyo mwaka huu, waligomea kucheza mechi yao ya pili mfululizo leo Jumanne.

Kutokana na hayo Rais wa Ligi ya Mpira wa Kikapu Afrika (BAL) Amadou Gallo Fall leo ametoa taarifa kuhusiana na uamuzi wa Klabu hiyo ya Burundi wa kukataa kushiriki katika msimu wa mwaka 2024 wa BAL.

"Klabu ya Mpira wa Kikapu ya Dynamo imekataa kufuata kanuni na matakwa ya Ligi ya Mpira wa Kikapu Afrika-BAL kuhusu jezi na hivyo kupoteza mchezo wake wa leo dhidi ya Petro de Luanda ya Angola na ushiriki wake katika msimu wa 2024 wa BAL.

Chini ya sheria za FIBA,kukosa mechi mbili katika michuano hiyo husababisha klabu kujiondoa yenyewe moja kwa moja.

Hii ni hali ya kusikitisha sana kwa wachezaji na mashabiki nakila mtu anayehusika amesikitishwa.

Michezo yote iliyosalia ya Kanda ya Kalahari itachezwa jinsi ilivyoratibiwa, na tunatazamia kuwashirikisha mashabiki mjini Pretoria kupitia matukio mengi ya mashabiki na jamii” aliongeza.

Baadhi ya taarifa katika hii ripoti inatokana na shirika la habari la Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG