Wawakilishi wa Burundi katika michuano ya mwaka huu ya Ligi ya Mpira wa Kikapu Afrika- BAL katika mashindano yanayofadhiliwa na Chama cha mpira wa Kikapu NBA tawi la Afrika Jumatatu walipoteza ushiriki wao baada ya kukataa kuvaa jezi yenye nembo ya Visit Rwanda.
Timu ya Morocco FUS de Rabat imeifunga timu ya Angola ya Petro de Luanda 82 – 73 katika ufunguzi wa michuano ya msimu wa Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Afrika (BAL) 2024.
Timu ya Al Ahly ya Misri imetawazwa kuwa mabingwa wa ligi ya mpira wa kikapu barani Afrika BAL baada ya kuifunga AS Douanes ya Senegal kwa jumla ya pointi 80 kwa 65 siku ya Jumamosi mjini Kigali.
Ligi maarufu zaidi duniani katika mpira wa kikapu NBA inayochezwa Marekani ina mchakato mpana wa kuwatambua na kuwashirikisha vijana walio na vipaji katika mchezo huo.
Sherehe za ufunguzi wa Ligi ya Mpira wa Kikapu Afrika BAL mjini Kigali, Rwanda ambayo ni wenyeji wa fainali za msimu wa tatu. Michuano ya msimu huu ilianza Machi 11, 2023 na itamalizika Mei 27, 2023,
Timu nane zilizofanikiwa kuingia robo fainali ya klabu bingwa barani Afrika - BAL ya mwaka 2023 sasa zinajulikana kufuatia kumalizika kwa kanda ya Nile iliyofanyika Cairo, Misri.
Katika michuano ya ligi ya klabu bingwa ya ligi ya mpira wa kikapu barani Afrika kanda ya Nile katika uwanja wa Hassan Mostapha indoor Complex timu za Petro de Luanda ya Angola na Ferroviario da Beira ya Msumbiji walipambana Jumamosi.
Timu ya Uganda City Oilers ilijikuta inaanguka kwa mara ya pili baada ya kufungwa na mabingwa wa Guinea SLAC kwa jumla ya pointi 96 kwa 68.
Timu ya ABC ya Ivory Coast iliongeza nafasi yake ya kufuzu kwenye robo fainali ya ligi ya mpira wa kikabu Afrika kwa ushindi wa jumla wa pointi 79 -76 katika mchezo mkali dhidi ya Falcon ya Nigeria. Ungana na mwandishi wetu akukuletea yaliyojiri katika mchezo huo...
Timu ya Stade Malien ya Mali imeibuka na ushindi wa pointi 84 kwa 64 dhidi ya mabingwa wa Rwanda Rwanda Energy Group (REG) katika mchezo wa kwanza siku ya Jumamosi huko Dakar Arena Senegal.
Timu ya Abidjan Basket Club (ABC) iliwashangaza mabingwa watetezi wa BAL US Monastir ya Tunisia siku ya Ijumaa na kuongeza uwezekano wao wa kufuzu kwenda robo fainali ya michuano hiyo mwezi Mei mjini Kigali.
Msimu wa tatu wa BAL unaendelea huko Senegal.Timu 6 kutoka nchi 4 ziko Dakar zikicheza raundi ya kwanza kutafuta nafasi ya kwenda kwenye fainali zitakazofanyika Kigali.
Pandisha zaidi