Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 09:53

Stade Malien ya Mali waiangusha REG ya Rwanda


Jean Jacques wa Rwanda Energy Group akiambaa na mpira wakati wa mchezo dhidi ya US Monastir ya Tunisia.(Picha na Pape Emir/NBAE kupitia Getty Images).
Jean Jacques wa Rwanda Energy Group akiambaa na mpira wakati wa mchezo dhidi ya US Monastir ya Tunisia.(Picha na Pape Emir/NBAE kupitia Getty Images).

Timu ya Stade Malien ya Mali imeibuka na ushindi wa pointi 84 kwa 64 dhidi ya mabingwa wa Rwanda Rwanda Energy Group (REG) katika mchezo wa kwanza siku ya Jumamosi huko Dakar Arena Senegal.

Timu ya Stade Malien ya Mali imeibuka na ushindi wa pointi 84 kwa 64 dhidi ya mabingwa wa Rwanda Rwanda Energy Group (REG) katika mchezo wa kwanza siku ya Jumamosi huko Dakar Arena Senegal.

Mchezaji wa Souleymane Barthe aliiongoza timu ya Mali kwa kupachika jumla ya pointi 23 akifuatiwa na Aliou Diarra pointi 20 na kupachika rebaundi 16 kuweka Kelvin Amayo pointi 14. Wakati kwa upande wa Rwanda Energy Group Adonis Filer aliongoza timu hiyo kwa kupachika pointi 19 na mchezaji delwan Graham pointi 18 na Cleveland Thomas Jr alijipatia pointi 6 na assisti 10 wakati mchezajiw a chuo cha NBA Afrika Ulrich Kaka Chomche alijipatia pointi 9.

Na mchezaji hatari wa REG Dieudonne Ndayisaba Ndizeye alijipatia pointi 8 .

Mabingwa hawa wa Mali walijhitaji ushindi wa mechi hii kwa kiasi kikubwa kwani wangepoteza mchezo huu basi wamngekuwa wametolea katika michuano hii baada ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya AS Douanes ya Senegal kwa jumla ya pointi 74-58.

Mshambuliaji wa Rwanda Energy Group (REG) Cleveland Thomas Jr alifunga pointi mbili za kwanza katika mchezo huo.

Lakini Aliou Diarra hakuchukua muda mrefu kujibu, na kufunga moja ya mipira yake miwili ya adhabu kupunguza pengo hadi 2-1, kabla ya kufunga pointi mbili nyingine na kuendelea kuiweka Stade Malien mbele kwa muda wote wa mchezo huo.

Ushindi wa Stade Malien wa 84-64 dhidi ya REG haumaanishi tu kwamba wamerejea kwenye kinyang'anyiro cha kufuzu, lakini pia ulihitimisha mfululizo wa ushindi wa mabingwa hao wa Rwanda katika michezo mitatu mfululizo.

Hata hivyo timu ya REG pamoja na kupoteza mchezo huu tayari imeshafanikiwa kuingia robo fainali ya michuano hii itkayofanyika huko Kigal Rwanda.

XS
SM
MD
LG