Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 13:33

Al Ahly yatwaa ubingwa wa BAL 2023


Mchezaji wa Al Ahly Anunwa Omot akipachika mpira nyavuni dhidi ya Capetown Tigers katika ligi ya BAL kanda ya Nile. (Picha na NBAE/Getty Images)
Mchezaji wa Al Ahly Anunwa Omot akipachika mpira nyavuni dhidi ya Capetown Tigers katika ligi ya BAL kanda ya Nile. (Picha na NBAE/Getty Images)

Timu ya Al Ahly ya Misri imetawazwa kuwa mabingwa wa ligi ya mpira wa kikapu barani Afrika BAL baada ya kuifunga AS Douanes ya Senegal kwa jumla ya pointi 80 kwa 65 siku ya Jumamosi mjini Kigali.

Baada ya kipindi cha kwanza cha mabao machache mpaka kufikia mapumziko timu ya Al Ahly ilielekea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo ikiwa mbele kwa jumla ya pointi 38-33.


Katika kota ya tatu wachezaji Corey Webster na Ehab Amin waliiongoza Al Ahly kwa jumla ya pointi 57-44. Nuni Omot aliiongoza Al Ahly, akimaliza mchezo akiwa na jumla ya pointi 22 na Corey Webster pointi 13 akitokea kwenye benchi.

Nuni Omot alitajwa kuwa mshindi wa tuzo ya MVP ya mwaka 2023 ya Hakeem Olajuwon. Al Ahly imekuwa timu Misri ya pili kushinda michuano ya BAL tangu Zamalek iliposhinda msimu wa kwanza wa BAL

Al Ahly walihitimisha kampeni yao ya BAL mwaka 2023 kwa rekodi ya jumla ya ushindi wa 7-1.

Na kwa ushindi huo Al Ahly sasa wataiwakilisha Afrika katika toleo linalofuata la FIBA Intercontinental Cup.

Forum

XS
SM
MD
LG