Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 17:48

Timu ya ABC yawashangaza mabingwa watetezi wa BAL US Monastir

Kocha wa mpira wa Kikapu wa Australia Liz Mills, aliyeajiriwa kufundisha ABC Fighters ya Ivory Coast ambapo mwaka jana alikuwa na Klabu ya AS Sale ya Morocco ndiye kocha mkuu wa kwanza wa kike wa BAL. (VOA).

Timu ya Abidjan Basket Club (ABC) iliwashangaza mabingwa watetezi wa BAL US Monastir ya Tunisia siku ya Ijumaa na kuongeza uwezekano wao wa kufuzu kwenda robo fainali ya michuano hiyo mwezi Mei mjini Kigali.

Wachache walitarajia timu hii inayocheza kwa mara ya kwanza katika michuano ya BAL -ABC kuifunga US Monastir ya Tunisia kwa jumla ya pointi 90-74, lakini mabingwa hao wa Ivory Coast hawakuangalia jina la timu au iadi ya michezo waliyoshinda au historia ya mabingwa hao na kusababisha mshangao mkubwa katika kanda ya Sahara hadi sasa.

Liz Mills, mwanamke wa kwanza kufundisha katika michuano ya BAL, ambaye sasa yuko katika msimu wa pili na timu hii alikiri kwamba wachezaji wake walifanya kazi ya ziada.

Mwaka jana alifundisha na timu ya AS Sale ya Morocco.

Kwa ushindi huo, ABC ilimaliza mfululizo wa ushindi wa mechi tano za Monastir za BAL wa Marekani uliodumu tangu Machi 2022.

"Tunajua kuwa siku yoyote tukicheza hivi tutashinda timu yoyote kwenye michuano ya BAL," Mills aliongeza.

Abdoulaye Harouna aliiongoza ABC kwa pointi zake 33; Mike Fofana alitengeneza pointi tatu mara 4 kati ya 7 na kumaliza na pointi 18 naye Stephane Konate alichangia pointi 15 katika ushindi huo.

Ulikuwa ni mchezo ambao ABC ilihitaji sana kushinda, na kuongoza 41-36 wakati wa mapumziko kulionyesha hali ya kutaka ushindi kwa kila hali kwa timu hii ya ABC.

Siku chache zilizopita, timu ya Monastir ilikuwa nyuma dhidi ya Kwara Falcons ya Niheria wakati wa mapumziko, lakini waliweza kubadilisha matokeo na kushinda mchezo huo katika kota ya mwisho.

Kwa kushinda mchezo huu ABC wamefufua matumaini yao ya kwenda robo fainali ya michuano hii .

XS
SM
MD
LG