Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 02:58

Je, radio itaendelea kuwa chombo cha habari kinachoaminiwa na kutumiwa zaidi?


Mwanamke mkimbizi akiwa amebeba redio akiwa kwenye ufukwe wa ziwa Tanganyika Picha na REUTERS/Thomas Mukoya
Mwanamke mkimbizi akiwa amebeba redio akiwa kwenye ufukwe wa ziwa Tanganyika Picha na REUTERS/Thomas Mukoya

Kauli mbiu ya Siku ya Radio Duniani mwaka 2024 inaangazia kwa upana mafanikio ya radio yaliyofikiwa siku za nyuma, uhalisia wake hivi sasa na maendeleo ya mustakbali wake.

Fursa iliyoletwa na mafanikio ya miaka zaidi ya 100 ya radio inatutaka tuitangaze kwa sauti kubwa.

Miaka 100 ni Tukio la Fahari

Miaka mia moja ni tukio la kuona fahari kusherehekea maadili mapana ya chombo hicho na uwezo wake unaoendelea kunufaisha umma.

Siku hii inafanyika wakati muafaka, ambapo Radio – licha ya kuwa kitakwimu inawashiriki wengi na kuaminika na umma – imekuwa ikiendelea kukabiliwa na changamoto kadhaa kwa wasikilizaji na idadi ya mapato kutokana na mitandao ya kidigitali, mitandao ya kijamii isiyopumzika, mgawanyiko wa kidigitali na vizazi, wimbi la udhibiti na, katika baadhi ya vyombo vya habari, kulazimika kukabiliana na madeni na hali ngumu ya kiuchumi iliyochochewa na soko la matangazo la mitandaoni.

Sherehe za Mwaka 2024

Mambo yanayo angaziwa wakati wa sherehe za mwaka 2024

Historia isiyosahaulika ya radio na matokeo yake yenye nguvu kwa upande wa habari, maigizo, muziki na michezo …

Radio inaendelea kuwa chombo muhimu kilicho huru na kuweza kutumika kwa urahisi kwa ajili ya usalama wa umma wakati wa matukio ya dharura na kukatika kwa umeme yanayotokea kwa majanga asilia au yaliyo sababishwa na mwanadamu kama vile vimbunga, matetemeko ya ardhi, mafuriko, joto, moto wa misituni, ajali na vita.

Umuhimu wa Radio katika Demokrasia

Umuhimu wa Radio katika kuendeleza demokrasia kwa kuhudumia kama kichocheo cha ngazi ya chini kuunganisha makundi ambayo yameachwa nyuma ikiwemo wahamiaji, dini, waliowachache na jamii zinazokumbwa na umaskini; na ikiwa ni chombo cha haraka kinachoongoza katika kufikisha maoni yaliyotolewa kupitia majukwaa ya uhuru wa kujielezea katika eneo la umma.

Ilitangazwa mwaka 2011 na nchi wanachama wa UNESCO, na kupitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 2012 kama Siku ya Kimataifa ya UN, Februari 13 ikawa Siku ya Radio Duniani (WRD).

Nguvu za Radio katika Kulinda Ubinadamu

Radio ni chombo chenye nguvu kwa ajili ya kusherehekea ubinadamu katika mchanganyiko wake wote na inaweka jukwaa kwa ajili ya mijadala ya kidemokrasia.

Katika ngazi ya kimataifa, radio inaendelea kutumika zaidi. Huu uwezo wake wa kipekee kuwafikia watu wengi zaidi inamaanisha kuwa radio inaweza kutengeneza uzoefu wa mchanganyiko katika jamii, ikiwa ni uwanja kwa sauti zote kutoa maoni yao, kuwakilishwa na kusikika.

Vituo vya Radio Vinawajibu Gani?

Vituo vya Radio vinatakiwa kuhudumia jamii za tabaka mbali mbali, zikiwapa programu mbalimbali, maoni mbalimbali na maudhui, na kuonyesha mchanganyiko wa makundi mbalimbali katika jumuiya zao na operesheni zao.

Radio inaendelea kuwa moja ya vyombo vya habari vinavyoaminiwa na kutumiwa zaidi ulimwenguni, kulingana na ripoti mbalimbali za kimataifa.

Nini sababu za msingi juu ya wazo la siku ya redio Duniani?

Siku ya Radio Duniani (WRD) ilitangazwa na Mkutano Mkuu wa UNESCO katika kikao chake cha 36 mwaka 2011 na kupitishwa na kikao cha 67 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 2012.

Tarehe ilichaguliwa ilikuwa Februari 13, ambayo ni siku ya kuadhimisha kuundwa kwa Radio ya Umoja wa Mataifa mwaka 1946.

Nini Lengo la Siku ya Radio Duniani?

Siku ya Radio Duniani ni fursa ya kusherehekea radio kama chombo cha mawasiliano.

Ni fursa ya kuhamasisha ushirikiano wa kimataifa kati ya watangazaji wa radio, kuhimiza mitandao mikuu na stesheni mbalimbali za radio ndani ya nchi kujenga uwezo wa kupata habari na uhuru wa kujielezea.

Siku ya Radio Duniani ina malengo kadhaa, kuongeza uelewa kati ya umma na vyombo vya habari juu ya thamani ya huduma ya sauti kwa umma; kuwapa moyo wanaofanya maamuzi kuhamasisha uhuru, kujitegemea, na radio kwa wote kuanzishwa na kuiimarisha mitandao na ushirikiano wa kimataifa kati ya watangazaji.

Baadhi ya habari hii inatokana na Shirika la Umoja wa Mataifa la UNESCO

Forum

XS
SM
MD
LG