Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 06:26

Vyombo vya utangazaji vya upinzani Uturuki, kuchunguzwa


Waangalizi wa vyombo vya utangazaji vya Uturuki, Jumanne, wametangaza kuchunguza vituo sita vya televisheni vya upinzani kwa madai ya ‘kutukana umma’ kupitia matangazo ya duru ya pili ya uchaguzi wa rais wa Jumapili.

Baraza Kuu la Radio na Televisheni, ama RTUK, limesema watazamaji walilalamika kuhusu matangazo ya uchaguzi lakini hawakutoa mifano kamili.

Kituo kimoja kinacho-chunguzwa, kimesema kupitia tovuti yake kwamba hatua hiyo inaonyesha namna serekali inavyobana kituo hicho na kazi zake.

Madai hayo yametokea siku mbili baada ya rais Tayyip Erdogan wa chama cha haki na maendeleo ama AKP kutangazwa mshindi wa uchaguzi baada ya kufanyika duru ya pili ya uchaguzi wa rais Jumapili.

Kamati ya kulinda wanahabari imedai kwamba ukiukwaji wa uhuru wa vyombo vya habari ulifanyika na kabla uchaguzi wanahabari kadhaa walikamatwa, kushikiliwa jela na kudhalilishwa kwa kuripoti uchaguzi.

Forum

XS
SM
MD
LG