Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 16:39

Kiongozi wa radio Gorilla FM DRC  ashambuliwa na watu wenye silaha


Makasha ya risasi yakionekana baada ya kiongozi wa wanahabari Egide Kitumaini katibu wa chama cha waandishi wa habari -UNPC huko South Kivu, kushambuliwa na watu wenye silaha.
Makasha ya risasi yakionekana baada ya kiongozi wa wanahabari Egide Kitumaini katibu wa chama cha waandishi wa habari -UNPC huko South Kivu, kushambuliwa na watu wenye silaha.

Kiongozi wa redio Gorilla FM Egide Kitumaini ambaye pia ni Katibu wa Umoja wa Wanahabari wa Congo-UNPC Kivu Kusini  ameshambuliwa na watu wenye silaha muda mfupi baada ya kurudi nyumbani kwake jioni.

Watu wawili waliingia ndani nawengine 4 walibaki nje. Tulionana nao wala hawakuficha nyuso zao, mmoja kati yao alikuwa na silaha ya AK 47 mkononi sijui kwanini hakunifyatulia papo hapo alipoingia. Hapo nilipambana nao hadi jikoni na hapo walifyatua risasi mara tatu, moja imenipita kati ya vidole. Mara watoto walipolalamika waliondoka haraka ila wamepeleka vyombo vyangu vya kazi. Lakini inaonekana kwamba mmoja alimfyatulia mwingine risasi kwani kuna damu nyia yote waliopitia” alisema Kitumaini.

Katika tarifa kwa vyombo vya habari, Muungano wa wanahabari katika jimbo la Kivu kusini umelaani shambulizi hilo ukihakikisha kwamba ni kitendo cha kinyama. Muungano wa wanahabari wa jimbo la Kivu kusini unazitaka mamlaka kujihusisha na sulala hili na kuhakikisha usalama wa wanahabari wakati huu kunapopangwa uchaguzi nchini Congo.

"Wametamka kinywani mwao kwamba wamekuja kumuuwa na basi awape kila alicho nacho. Tunaomba wakuu watusaidie kutafuta wale watu. Sheria ya Congo iwafuatilie” alisema Darius Kitoka msimamizi wa muungano huo.

Shambulizi hilo limefanyika muda mfupi baada ya shambulizi lingine dhidi ya mwanasheria Maurice Mirindi, mtetezi wa haki za kibinadamu kutoka Shirika linalotetea haki na amani ICJP mjini Bukavu.

Katika taarifa nyingine, Shirika lingine la utetezi wa haki za kibinadamu linaloitwa Ushirikiano kwa ajili ya ulinzi Jumuishi - PPI linatoa pia malalamiko. Jonathan Makoma anasimamia shirika hili mjini Bukavu akinyooshea kidole utawala wa sasa unaoshindwa kulinda raia wake.

Nchi inapokaribia kwenye uchaguzi tunagundua kwamba mambo yanazidi kuharibika. Wale waliopaswa kutetea haki au kujulisha wakazi habari ndio wanazidi kuathirika. Ni wajibu wa viongozi kulinda usalama wa wanahabari na watetezi wa haki za binadamu" alisema Jonathan Makoma, Msimamizi wa PPI Kivu kusini.

Utawala haujaeleza kuhusu mashambulizi hayo. Hata hivyo, Msemaji wa chama tawala cha UDPS anasema juhudi zinafanyika.

Umoja wa wanahabari UNPC umeahidi kuwafungulia mashitaka wale wote ambao wametoa vitisho kwa njia yoyote ile dhidi ya wanahabari ikiwemo hata kupitia mitandao ya kijamii.

Imeandaliwa na Mitima Delachance, Bukavu.

Forum

XS
SM
MD
LG