Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 02, 2025 Local time: 17:11

Tiketi za Michezo ya Olimpiki milioni tisa Paris zauzwa chini ya euro 50 kila moja


Fuatilia Michezo ya Olimpiki Paris 2024 kupitia VOA Swahili. Taarifa za michezo hiyo zitaanza kutolewa Julai 26, 2024.
Fuatilia Michezo ya Olimpiki Paris 2024 kupitia VOA Swahili. Taarifa za michezo hiyo zitaanza kutolewa Julai 26, 2024.

Takriban tikiti milioni tisa tayari zimeuzwa - milioni sita kati yao kwa chini ya Euro 50.

Mashabiki wanaweza kufurahia matukio kama vile baiskeli barabarani, triathlon au mbio za marathon, ambazo ni wazi kwa wote.

Umma unaweza kushiriki katika matukio, kama vile "Marathon Pour Tous" ambapo watu 40,000 watakimbia kwenye njia ya washiriki wa Olimpiki saa chache kabla ya wanariadha hao wa Olimpiki kuanza mashindano yao.

Mamilioni ya watoto wa Ufaransa tayari wanashiriki katika mazoezi ya kila siku kama sehemu ya mtaala wao wa shule.

Tayari michuano hiyo imeshaandaliwa kwa Michezo ya Olimpiki ambayo itakuwa ya vijana zaidi, jumuishi zaidi na endelevu zaidi. Itakuwa Michezo ya kwanza ya Olimpiki ambayo inawiana kikamilifu na mageuzi ya Ajenda ya Olimpiki ya IOC kuanzia mwanzo hadi mwisho. Hii itakuwa Michezo ya Olimpiki ambapo kila mtu anaweza kushiriki sehemu yake, si tu kama watazamaji, lakini pia kama washiriki.

Ufunguzi wa michuano ya Olimpiki 2024 unazidi kukaribia ambapo michuano hiyo inatarajiwa kuanza Julai 24 huko Paris ufaransa

Tayari mamilioni ya watu wameupokea mwenge wa Olimpiki katika safari yake ya kuzunguka Ufaransa kwa shauku kubwa.

Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali vya habari.

Forum

XS
SM
MD
LG