Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 06, 2024 Local time: 10:35

Meya wa Paris aogelea katika mto Seine kuthibitisha unafaa kutumiwa katika Olimpiki


Meya wa Paris Anne Hidalgo akiongelea katika mto, Julai 17, 2024 in Paris.
Meya wa Paris Anne Hidalgo akiongelea katika mto, Julai 17, 2024 in Paris.

Meya wa Paris, Anne Hidalgo, aliogelea katika maji yenye matope ya Seine Jumatano kuonyesha kuwa mto huo hivi sasa ni msafi kabisa kwa ajili ya matukio ya kuogelea wakati wa michezo ya Olimpiki.

Akiwa amevaa miwani maalum ya kuogelea na nguo za kuogelea, kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 65 aliogelea kifudifudi kabla ya kuuzamisha uso wake na kutambaa ndani ya maji, akikamilisha takriban mita 100 kwenda na kurudi katika mto huo.

Wananchi wakiogelea katika mto Seine baada ya Meya wa Paris Anne Hidalgo kuonyesha mfano, Julai 17, 2024, huko Paris, France.
Wananchi wakiogelea katika mto Seine baada ya Meya wa Paris Anne Hidalgo kuonyesha mfano, Julai 17, 2024, huko Paris, France.

Alikuwa ameogelea akiwa na maafisa wa ngazi ya juu na Tony Estanguet, mshindi wa medali ya dhahabu mara tatu katika mashindano ya kuendesha mtumbwi, anayeongoza kamati ya maandalizi ya Michezo ya Paris, itakayo funguliwa wiki ijayo Julai 26.

“Leo ni uthibitisho kuwa tuko pale ambako tulitarajia kuwa,” Estanguet alisema. “Hivi sasa tuko tayari kuandaa michezo hiyo huko Seine.”

Licha ya uwekezaji wa euro bilioni 1.4 ($1.5 bilioni) kuzuia maji taka kuvuja na kuingia katika mto huo, wasiwasi kuhusu mto huo umeenea katika jimbo la Seine kuelekea Michezo ya Paris.

Lakini kuanzia mwezi Julai, kutokana na mvua kubwa hatimaye kumekuwa na hali ya hewa ya joto, sampuli zikionyesha mto huo uko tayari kwa ajili ya uogeleaji na mashindano ya Olimpiki.

Forum

XS
SM
MD
LG