Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 06:19

Wakulima Kenya kufidiwa baada ya kupewa mbolea ghushi


FILE - Wakulima wakilima vitunguu katika eneo lililotengwa kwa kilimo karibu na Kimana Sanctuary huko Kimana, Kenya, Machi 2, 2021.
FILE - Wakulima wakilima vitunguu katika eneo lililotengwa kwa kilimo karibu na Kimana Sanctuary huko Kimana, Kenya, Machi 2, 2021.

Wakulima nchini Kenya waliopewa mbolea ghushi watafidiwa na serikali ya Kenya baada ya kampuni moja kutajwa kuwahadaa wakulima na hivyo kuiweka serikali katika hali ngumu kufuatia Sakata hilo.

Aidha serikali Alisema itapunguza zaidi bei ya mbolea ili kuwanufaisha wakulima.

Suala la Mbolea limekuwa moja ya suala kuu katika ajenda ya Rais William ruto hasa wakati wa kampeni ya mwaka 2022 kabla ya kupata ushindi.

Ruto alikuwa alizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha Clinker cha Cemtech Limited, eneo la Pokot Magharibi.

Hapo awali, Rais alifanya ziara ya ghafla katika Bohari ya Kitaifa ya Nafaka na Mazao (NCPB) mjini Eldoret.

Ruto aliagiza usimamizi wa NCPB kote nchini kuharakisha usambazaji wa mbolea ya ruzuku.

Mkuu huyo wa nchi aliendelea kusema kuwa walaghai wanaouza mbolea bandia watachukuliwa hatua.

Rais alitoa onyo kali kwa watu waliohusika akisema wanaofanya biashara hiyo haramu watakamatwa na kufunguliwa mashtaka.

Forum

XS
SM
MD
LG