Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 00:20

Madaktari Kenya wanaendelea na mgomo ulioanza takribani wiki 3 sasa


Madaktari Kenya wakiwa katika mgomo unaodai maslahi bora kazini.
Madaktari Kenya wakiwa katika mgomo unaodai maslahi bora kazini.

Madaktari wanaofanya kazi katika hospitali zinazoendeshwa na serikali ya Kenya, leo Alhamisi walikataa pendekezo la serikali linalolenga kumaliza mgomo wa wiki tatu, wakati mahakama ya kazi ikiweka tarehe ya mwisho kwa mzozo huo kutatuliwa.

Wanachama wapatao 7,000 wa muungano wa Chama cha Madaktari Kenya, Wafamasia na Madaktari wa meno (KMPDU) walifanya maandamano katikati ya mwezi Machi kudai malipo bora na mazingira mazuri ya kazi.

Mahakama ya kazi jijini Nairobi ilisitisha mgomo huo mwezi uliopita na Jumatano iliamuru mazungumzo ya kumaliza mgomo huo yakamilike ndani ya siku 14, vyombo vya habari nchini humo vimeripoti.

Uamuzi huo umekuja siku moja baada ya serikali kusema itatimiza baadhi ya matakwa ya madaktari, ikiwa ni pamoja na kulipa malimbikizo na kuajiri madaktari wanafunzi kwa mikataba ya kudumu, miongoni mwa malalamiko makuu.

Forum

XS
SM
MD
LG