Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 00:22

Madaktari wa Kenya waendelea na mgomo wa kitaifa


Baadhi iya madaktari wanaoshiriki mgomo nchini Kenya. Machi 4. 2024
Baadhi iya madaktari wanaoshiriki mgomo nchini Kenya. Machi 4. 2024

Madkatari kutoka hospitali za umma nchini Kenya ambao wamekuwa kwenye mgomo wa kitaifa tangu mwezi uliopita, Jumanne wamekusanyika kwenye miji mwili mikubwa, ili kushauriana kuhusu malalamiko yao dhidi ya serikali.

Muungano wa madaktari, wauza dawa na madakrati wa meno, KMPDU, ambao unawakilisha zaidi ya wanachama 7,000 uliitisha mgomo Machi 15, ili kudai mishahara iliyocheleweshwa, pamoja na kupewa ajira mara moja kwa madaktari wanafunzi.

Malalamiko yao ni kuanzia 2017 ambapo kulikuwa na makubaliano kati ya serikali na muungano huo. Madaktari hao pia wanataka bima ya afya kwa ajili yao na familia zao. Pia wanaiomba serikali ishugulikie tatizo la kucheleweshwa mara kwa mara kwa mishahara yao, pamoja na kutambuliwa kwa madaktari wanaofanya kwenye hospitali za umma kulingana na elimu yao.

Waziri wa afya Susan Nakhumicha amesema kwamba serikali kwa sasa haina uwezo wa kuajiri madaktari wanafunzi kutokana na uhaba wa fedha kwenye mfuko wa umma. Sekta ya afya nchini humo, ambayo madaktari wanasema haipewi fedha za kutosha, wakati pia ikiwa na wafanyakazi wachache, imekuwa ikikumbwa na migomo ya mara kwa mara.

Mazungumzo kati ya serikali na madaktari hao ili kumaliza mgomo huo hayajafanikiwa kufikia sasa, wakati maafisa wengine wa afya wakijiunga na mgomo, vyombo vya habari vimeripoti leo Jumanne.

Forum

XS
SM
MD
LG