Mwanahabari na mwanaharakati Maria Sarungi hatimaye amevunja ukimya kufuatia jaribio la kumteka nyara siku ya jumapili Nairobi, Kenya
Rais wa Kenya, William Ruto, Jumanne amekiri ukiukaji unaofanywa na vikosi vya usalama vya Kenya, kufuatia maandamano dhidi ya wimbi la karibuni la tuhuma za utekaji ambalo limezua ghadhabu nchini humo.
Rais wa Kenya William Ruto ameahidi kukomesha vitendo vya utekaji nyara ambavyo vimeongezeka siku za hivi karibuni na kulaaniwa na makundi ya kutetea haki za binadamu, wanasheria na wanasiasa.
Watoto 27 wamezaliwa hospitali nchini Kenya siku ya Krismas. Kati ya watoto hao, kumi ni wa kiume na 17 ni wa kike. Watoto hao walizaliwa na wanawake walio kati ya umri wa miaka 16 hadi 37.
Mwanasiasa maarufu wa upinzani wa Uganda alikamatwa wakati wa uzinduzi wa kitabu nchini Kenya mwishoni mwa wiki na kusafirishwa hadi Uganda, anashikiliwa katika jela ya kijeshi mjini Kampala, mke wake amesema leo katika mtandao wa kijamii wa X.
Huldah Momanyi Hiltsley aliweka historia hapo Novemba 5 alipokua mhamiaji wa kwanza mzaliwa wa Kenya kuchaguliwa mbunge wa jimbo la Minnesota.
Halmashauri ya Utendaji ya Shirika la Fedha Duniani, IMF imeidhinisha tathmini ya 7 na ya 8 ya programu ya Kenya, hatua ambayo IMF imesema itafungua njia kuelekea kupata mkopo wa dola milioni 606.
Rais wa Kenya Dr. William Ruto amekutana na mkurugenzi wa idara ya ujasusi ya Marekani CIA William Burns katika kikao ambacho kilihudhuriwa na mkuu wa ujasusi wa Kenya Noordin Haji.
Je, unafahamu namna ya kusaidia watu wenye kukata tamaa, kutokana na ulemavu au maradhi ya akili.
Kenya ilisema Jumatatu imewakabidhi wakimbizi wanne raia wa Uturuki baada ya kukubali ombi la Ankara la kutawaka warejeshwe nchini kwao
Naibu Rais wa Kenya Rigathi Gashagua atakabiliana na Seneti katika kesi ya kutaka kuondolewa madarakani, baada ya mahakama ya juu mjini Nairobi, Kenya kukataa kutoa maagizo ya kuizuia Seneti kuendelea na mjadala.
Kenya imeanza kuhamisha ndovu kutoka kwenye mbuga ya kitaifa ya wanyamapori ya Mwea, iliyopo mashariki mwa Nairobi baada ya idadi yao kuongezeka kutoka 50 hadi 150, na kwa hivyo kulemea mbuga hiyo yenye ukubwa wa kilomita 42 mraba.
Pandisha zaidi