Vikosi vya usalama katika taifa hilo la Afrika Mashariki vimeshutumiwa kwa kuwashikilia watu kadhaa kinyume cha sheria toka maandamano yaliyoongozwa na vijana dhidi ya serikali mwezi Juni na Julai kukandamizwa vikali.
Jumatatu, polisi waliwashikilia kwa nguvu mamia ya waandamanaji na kutumia gesi ya kutoa machozi katika mikutano midogo ya amani ya kutaka kuachiliwa kwa wale ambao waliotoweka.
Katiba hotuba yake ya mwaka mpya Rais Ruto amesema haiwezi kukanushwa kuwa kumekuwa na vitendo vya kupita kiasi na visivyo vya kisheria vya maafisa wa idara ya usalama.
Wiki iliyopita, rais anayekabiliwa na mzozo aliahidi kukomesha utekaji.
Forum