Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 04, 2025 Local time: 05:38

Ruto aahidi kukomesha vitendo vya utekaji nyara


Rais wa Kenya William Ruto
Rais wa Kenya William Ruto

Rais wa Kenya William Ruto ameahidi kukomesha vitendo vya utekaji nyara ambavyo vimeongezeka siku za hivi karibuni na kulaaniwa na makundi ya kutetea haki za binadamu, wanasheria na wanasiasa.

Maafisa wa usalama katika taifa hilo la Afrika Mashariki wamekuwa wakituhumiwa kuwashikilia kinyume cha sheria watu kadhaa tangu maandamano ya kuipinga serikali ya mwezi Juni na Julai mwaka huu.

Utekaji nyara wa hivi karibuni umewalenga zaidi vijana waliomkosoa Ruto kwenye mitandao ya kijamii, huku makundi ya kutetea haki za binadamu yakionekana kutokubaliana na polisi ambao wamekanusha kwamba hawahusiki katika utekaji nyara huo na kuomba hatua zichukuliwe.

Akizungumza mbele ya umati wa watu huko Homa Bay Ijumaa, Ruto aliahidi kukomesha vitendo vya utekaji nyara lakini aliwaambia pia wazazi kuwajibika katika malezi ya watoto wao.

“Tutakomesha utekaji nyara ili vijana waishi kwa amani,” alisema, kulingana na ripoti za vyombo vya habari nchini humo.

Forum

XS
SM
MD
LG