Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 02, 2025 Local time: 07:53

Sudan na wakosowaji walaumu Kenya kuruhusu kufanyika mkutano wa RSF


Wajumbe wanaounga mkono Kikosi cha Dharura cha Sudan RSF wakubaliana hoja wakati wa mkutano.
Wajumbe wanaounga mkono Kikosi cha Dharura cha Sudan RSF wakubaliana hoja wakati wa mkutano.

Serikali ya Kenya imkosolewa na mkuu wa jeshi la Sudan na baadhi ya wakosowaji wa nchi hiyo kwa kudai imefanya kitendo cha uhalifu wa kutowajibika kwa kuwaruhusu waasi wa kundi la wanamgambo wa Sudan RSF kukutana Nairobi na kupanga kutangaza serikali ya uhamishoni.

Wizara ya mambo ya nje ya Sudan ambayo inamtii Jenerali Abdel Fattah al-Burhan imeikosoa Kenya kwa kuruhusu mkutano huo kufanyika.

Katika taarifa yake Jumatano, wizara ya mambo ya nje ya Sudan imeikosoa vikali serikali ya Nairobi ikisema hatua hiyo inahamasisha kutenganishwa kwa mataifa ya Afrika, ikikiuka uhuru wa mipaka na kuingilia kati masuala ya ndani ya nchi.

Maafisa wa Kundi la wanamgambo wa Dharura la Sudan RSF wanaokutana Nairobi pamoja na vyama vya siasa na mashirika ya kiarai yanayo waunga mkono, waliahirisha hapo Jumanne utiaji saini mkataba wa kuunda serikali ya muungano uhamishoni, “kwa ajili ya amani na umoja” ambayo ingetawala maeneo kundi hilo linadhibiti.

Mwanasiasa Fadlallah Burma Nasir, kiongozi wa chama cha Umma kilichogawanyika kuhusu kushiriki au la kwenye mkutano huo wa Nairobi anasema utiaji saini umecheleweshwa hadi mwisho wa wiki ili kuwaruhusu kuwasili wajumbe kamili kutoka kiongozi wa kundi la waasi la SPLM-N Abdelaziz al-Hilu.

SPLM-N ni kundi la kijeshi linalodhibiti sehemu kubwa ya jimbo linalokabiliwa na njaa la Kordofan Kusini, na halijaunga mkono upande wowote wa vita kati ya jeshi la serikali na RSF.

Abdul Rahim Hamdan Dagalo (R), naibu kamanda wa RSF kakake Dagalo, akifuatana na mwenyekiti wa SPLA-North Abdelaziz al-Hilu (L), wakiwasili kwenye mkutano
Abdul Rahim Hamdan Dagalo (R), naibu kamanda wa RSF kakake Dagalo, akifuatana na mwenyekiti wa SPLA-North Abdelaziz al-Hilu (L), wakiwasili kwenye mkutano

Akiungana na RSF al-Hilu ataimarisha nguvu za kundi hilo la wanamgambo katika upande wa kudhibiti majimbo zaidi nchini humo.

"Tunataka kuunda taifa jipya, ambalo ni tofauti na Sudan ya zamani iliyokua chini ya misingi ya kutenganisha, ubaguzi, chuki rushwa na kadhalika."

Msemaji wa serikali ya Sudan Khalid Alesir, akizungumza pia na shirika la Habari la Reuters amekosoa uamuzi wa SPLM-N kujiunga na wanamgambo.

"Kundi la Abdelaziz al-Hilu imeonesha kuwa na uwamuzi dhaifu ilipojiunga na ajenda ya RSF, lakini tunafahamu kuna shinikizo kutoka nje kuwataka kuidhinisha ajenda hiyo."

Mjini Nairobi Rais William Ruto anakabiliwa na ukosoaji kutoka wanasiasa na mashirika ya kiraia.

Mwanasiasa na katibu mkuu wa zamani wa Shirika la Biashara Duniani, WTO, Mukhisa Kituyi ameliambia Shirika la Habari la AFP kwamba, kile Ruto anakifanya ni kuacha kando bila ya kujali utamaduni wa kuchukua tahadhari na mwelekeo wa busara wa sera za kidiplomasia za Kenya.

Ameongeza kusema kwamba anajaribu kuhalalisha genge linalowadhuru raia wake.

Ugomvi kati ya RSF na jeshi la serikali umeigawa Sudan ambapo jeshi linashikilia majimbo ya mashariki na kaskazini na RSF inashikilia maeneo yote ya magharibi na shehemu kadhaa za kusini, huku jeshi likifanya maendeleo ya kuwaondoa wanamgambo kutoka mji mkuu wa Khartoum na maeneo ya kati.

Kenya yalaumiwa kwa kuruhusu RSF kukutana Nairobi
please wait

No media source currently available

0:00 0:03:48 0:00

Forum

XS
SM
MD
LG