Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 23:51

Wanajeshi DRC wahukumiwa kifo kwa kukimbia vita


Wanajeshi wa jeshi la Congo wanaotuhumiwa kwa kosa la uasi na woga wakati wakipambana na waasi wa M23 wakiwa kizimbani Goma, Mei 03, 2024. Picha na MURHABAZI/AFP
Wanajeshi wa jeshi la Congo wanaotuhumiwa kwa kosa la uasi na woga wakati wakipambana na waasi wa M23 wakiwa kizimbani Goma, Mei 03, 2024. Picha na MURHABAZI/AFP

Mahakama ya kijeshi katika mji wa Goma huko Kivu Kaskazini Mashariki mwa Congo imewahukumu kifo maafisa nane wa jeshi la Congo, FARDC kwa tuhuma za kukimbia vita na kutoheshimu sheria za kijeshi.

Miongoni mwao ni Kanali Shamba mkuu wa kikosi cha makomandoo pamoja na msaidizi wake.

Mwendesha mashtaka amesema makamanda hao walishindwa kuwajibika kwenye uwanja wa mapambano karibu na mji wa Sake wilayani Masisi eneo lililo magharibi mwa mji wa Goma ambako M23 wanaendelea kuchukua udhibiti wa vijiji.

Wakili wa makamanda hao Bwito Jean Richard wa jeshi tiifu kwa serikali amesema mahakama imefanya makosa kutoa adhabu ya kifo kwa wanajeshi hao ambao walikuwa wamejitolea kulipigania taifa.

Hata hivyo amekata rufaa na kuionya Mahakama kuwa makini kwa kuwa hatua za mahakama zinaweza kuwapelekea wanajeshi wengi kutokwenda vitani.

Lakini baadhi ya wachambuzi wamesema hatua hii itawazuia wanajeshi kukimbia mapigano kila mara na kuwaacha waasi kuchukua vijiji.

Katika hukumu hiyo wanajeshi watatu, kapteni mmoja na maluteni wawili waliachiliwa huru na mahakama kwa madai ya kutokuwa na hatia.

Makamanda hao walipewa adhabu ya kifo kwa mujibu wa sheria ya nchi hiyo. Wakati huohuo Mkuu wa mahakama ameziomba pande husika kukata rufaa katika kipindi cha siku tano.

Imeandaliwa na Austere Malivika , Sauti ya Amerika Goma

Forum

XS
SM
MD
LG