Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 16:20

Wanadiplomasia waambiwa gharama za kumuokoa mtoto na ubakaji ni chini ya dola moja


Niemat Ahmadi, mwanzilishi na rais wa kundi la Darfur Women Action, baada ya kutoa ushahidi kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Aprili 23, 2024.
Niemat Ahmadi, mwanzilishi na rais wa kundi la Darfur Women Action, baada ya kutoa ushahidi kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Aprili 23, 2024.

Muigizaji na balozi wa ukarimu wa Umoja wa Mataifa Danai Gurira amewaambia wanadiplomasia siku ya Jumanne kuwa kumpata mtoto kutoka katika unyanyasaji wa kingono katika maeneo ya kivita kunagharimu chini ya dola moja.

Pia amewataka watunga sera kuzuia mtiririko wa silaha za magendo ikiwa njia moja ya kuzuia uhalifu huu.

“Senti themanini. Lini mara ya mwisho ulikuwa na senti 80?” mwigizaji na mwandishi huyo wa tamthilia wa Marekani mwenye asili ya Zimbabwe aliwauliza wajumbe wa Baraza la Usalama.

“Kulipia kitu ambacho gharama zake zote ni hizo tu? Kiwango hicho pia hakitoshi kununua pipi katika enzi hii, lakini kinaweza kumnunua mtoto kutoka katika kambi ya unyanyasaji wa kingono ya watu waliopoteza makazi inayoitwa maison de tolerance iliyoko Mashariki mwa DRC.

Umoja wa Mataifa umerekodi kesi zilizothibitishwa za ubakaji 3,688, ubakaji wa magenge na utekaji katika maeneo yenye vita mwaka 2023— ikiwa ni ongezeko la asilimia 50 katika kipindi cha mwaka 2022.

Takriban asilimia 70 mpaka 90 ya matukio hayo yanahusisha silaha ndogo ndogo na nyepesi. Karibu waathirika wote ni wanawake na wasichana. Manusura wengi hawajitokezi, kwa hiyo U.N inasema hii ni sehemu ya uhalisia wa idadi ya kweli.

Wanawake na wasichana wadogo wanateseka kutokana na kubakwa na unyanyasaji wa kingono katika mikono ya takriban mataifa 58 na makundi yenye silaha yasiyo ya kiserikali katika maeneo yenye migogoro duniani kote katika kipindi cha mwaka jana, Pramila Patten Mjumbe Maalumu wa U.N wa unyanyasaji wa kijinsia katika maeneo yenye mgogoro.

Amesema ripoti ya hivi punde ya ofisi yake inaangazia “kiwango kisicho na kawaida cha ukatili mkubwa” unaotumika kuwanyamazisha waliobakwa.

Amesema wale wanaowasaidia manusura mara nyingi wanateseka na ulipizaji visasi.

Forum

XS
SM
MD
LG