Wakiongozwa na waziri wa masuala ya jinsia, familia na watoto nchini humo, Gisele Ndaya, waandamanji hao walimebeba mabango yalionadikiwa matamshi mbali mbali kutaka mvita vimalizike,
Miongoni mwa waandamanaji hao ni pamoja na wanasiasa wanawake, na watumishi wa umma wakitoa shinikizo la kusitishwa kwa vita Mashariki mwa DRC na wakidai haki kwa takriban wahangaa millioni mbili walitokana na vita vita hivyo iliyoanza tangu mwaka 1994.
Wanawake hao waliva mavazi ya rangi nyeusi wakiandamana hadi katika Jengo la Ikulu ya rais, ambako waziri Gisele Ndaya aliwasilisha rasmi hati ya kushutumu kuhusika kwa Rwanda katika nchi yao na kupora mali asili ya DRC.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, vijana waliandamana katika mji mkuu wa Kinshasa wakitaka mataifa ya Magharibi na Umoja wa Mataifa kuondoka DRC wakiwashutumu kwa unyonyaji wa malia sili ya taifa hilo na kuwezesha mapigano kuendelea.
Forum