Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 24, 2024 Local time: 10:40

Jeshi la Rwanda linalotuhumiwa kuunga mkono M23 linatumia makombora ya kisasa


Waasi wa kundi la M23 wakati wa mkutano kati ya maafisa wa Kikosi cha Afrika Mashariki (EACRF) na waasi wa M23 katika kambi ya Rumangabo huko DRC Januari 6, 2023. Picha na Guerchom Ndebo/AFP
Waasi wa kundi la M23 wakati wa mkutano kati ya maafisa wa Kikosi cha Afrika Mashariki (EACRF) na waasi wa M23 katika kambi ya Rumangabo huko DRC Januari 6, 2023. Picha na Guerchom Ndebo/AFP

Jeshi la Rwanda linalo tuhumiwa kuunga mkono kundi la waasi la M23 huko Mashariki kwa Jamuhuri ya Kidemokratiki ya Congo, linatumia silaha za kisasa kama vile makombora ya kutoka aridhini kushambulia angani, kulingana na waraka wa Umoja wa Mataifa uliotolewa Jumatatu, wakati mapigano yakiongezeka.

Mapigano ya aridhini yanayopamba moto, mvutano unaongezeka zaidi katika Jamuhuri ya Kidemodrasia ya Congo.

Kombora linaloshukiwa limefyatuliwa kutoka kwenye gari kuelekea angani (SAM) na Jeshi la Ulinzi la Rwanda (RDF) " halikufanikiwa kutengua ndege ya upelelezi isiyokuwa na rubani ya Umoja wa Mataifa siku ya Jumatano, repoti hiyo ya siri ilisema.

Katika ripoti hiyo, picha mbili zilizopigwa kutoka angani zinaonesha gari la kivita lenye magurudumu sita lilionekana kupitia mfumo wa rada na jukwa la kufyetua makombora kwenye paa.

Picha hizo zilipigwa na ndege hiyo ilisiyokuwa na rubani iliyokuwa ikilengwa takriban kilomenta 70 Kaskazini mwa Goma, katika wilaya ya Rutshuru inayoshikiliwa na waasi.

Waraka huo umenukuu kuwa M23 na jeshi la Rwanda zinatumia silaha mbalimbali dhidi ya ndege na pia ndani ya magari yao ya kijeshi wana bunduki za kutungua ndege na mfumo wa ulinzi anga unaosafirishwa kwa gari wa MANPAD.

Silaha kama hizo zinasababisha hatari kubwa kwa serikali ya DRC na ndege za Umoja wa Mataifa, waraka huo umeeleza.

Mpaka sasa Umoja wa Mataifa na jeshi la DRC hawakutoa taarifa kuhusiana na tukio hilo.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG