Kulingana na vyanzo hivyo, siku ya Ijumaa waasi wa M23 waliliteka eneo la Shasha kwenye barabara inayounganisha miji ya Goma na Bukavu.
Tangu wakati huo, mji wa Minova ulioko kusini mwa barabara hiyo unapokea wakimbizi wengi wa ndani wanaokimbia kusonga mbele kwa waasi hao, mwakilishi wa mashirika ya kiraia huko Minova Delphin Birimbi ameliambia shirika la habari la AFP.
Wakitokea katika wilaya ya Masisi huko Kivu Kaskazini, wakimbizi hao wa ndani wameomba hifadhi katika nyumba za wakazi, shule na makanisa, Birimbi ameongeza.
“Waumini hawakwenda kanisani Jumapili kwa sababu ya hofu ambayo inazidi kuongezeka na kudumaza shughuli,” amesema mwandishi wa habari wa radio ya huko Minova.
Forum