Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 17:42

Polisi DRC yatawanya maandamano kwa mabomu ya kutoa machozi


Polisi wapambana na waandamanai Kinshasa
please wait

No media source currently available

0:00 0:00:28 0:00

Polisi wapambana na waandamanai Kinshasa

Polisi katika mji mkuu wa Kinshasa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wamefyatua gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji ambao wamechoma matairi ya gari na bendera za Marekani na Ubelgiji karibu na ubalozi wa nchi za Magharibi na ofisi za Umoja wa Mataifa.

Maafisa wa serikali wanasema hali ilirudi shuri kufikia mchana wa leo baada ya kuimarisha usalama kwenye ofisi hizo za nje za kigeni, baada ya maandamano na ghasia za siku tatu.

Waandamanaji wanashutumu nchi za Magharibi kwa kuisaidia nchi jirani ya Rwanda ambayo inalaumiwa kwa kusaidia uasi unaoongozwa na kundi la M23 la watutsi mashariki ya nchi.

Kundi hilo linaripotiwa kufikia karibu kilomita 5 kutoka mji muhimu wa Goma, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini, kufuatia mapigano yanayozidi kuongezeka .

Rwanda imekanusha tuhuma hizo. Hata hivyo, Congo, pamoja na serikali za Magharibi ikiwemo Marekani na Ubelgiji na taarifa kutoka kundi la kitalaamu la Umoja wa Mataifa zilionyesha kuwa kundi hilo la uasi linanufaika kutokana na msaada wa Rwanda.

Forum

XS
SM
MD
LG