“Mabomu” yalianguka kwenye vibanda ambavyo ni nyumba za wasiokuwa na makazi, kulingana na mashahidi, katika eneo la mashariki mwa nchi, ambalo limeshuhudia mapigano yanayoendelea kati ya waasi wa M23 na serikali.
Chanzo cha milipuko ya Ijumaa hakijafahamika wazi. Kwa mujibu wa mashahidi, wanajeshi wa serikali walio karibu na kambi hiyo wamekuwa wakiwashambulia waasi kwenye milima ya eneo la mbali magharibi mwa nchi tangu asubuhi, kulingana na mwanaharakati wa mashirika ya kiraia, “M23 walilipiza kisasi kwa kurusha makombora kiholela”.
Msemaji wa serikali Patrick Muyaya amelishutumu kwenye mtandao wa X “jeshi la Rwanda na waasi wa M23” kwa kuhusika na shambulio hilo.
Kulingana na serikali ya Congo, Umoja wa mataifa na nchi za Magharibi, nchi jirani ya Rwanda inawaunga mkono waasi wa M23, madai yanayokanushwa na Kigali.
Waasi wa M23 wamekanusha pia kwamba hawakuhusika na shambulio hilo na kulishtumu jeshi la DRC kwa kurusha mabomu hayo.
Forum