Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 09:13

JD Vance ajitambulisha na kueleza ajenda ya chama katika Kongamano la Republikan


JD Vance akihutubia Kongamano la Kitaifa la Chama cha Republikan Jumatano, Milwauke, Wisconsin, Marekani.
JD Vance akihutubia Kongamano la Kitaifa la Chama cha Republikan Jumatano, Milwauke, Wisconsin, Marekani.

Katika hotuba iliyosubiriwa kwa hamu kubwa na Wamarekani , hatimaye JD Vance alisimama mbele ya jukwaa kujitambulisha na kuelezea ajenda za chama cha Republican katika mkutano wa chama cha Republican unaokamilika hii leo Milwauke, Wisconsin.

JD Vance alijitosa kwenye ukumbi wa Fizer kutoa hotuba yake ya Kwanza tangu kuchaguliwa kama mgombea mwenza

J.D. Vance, Republican Vice Presidential Nominee anasema: “Tumeacha kuagiza wafanya kazi kutoka nje ya nchi. Tutapigania raia wa Marekani na kazi zao nzuri na mishahara yao mizuri.

Akiwa haijulikani kote Marekani, Vance mhitimu wa shule ya Yale Law ambaye alihudumu katika jeshi la Marekani kwa miaka sita -- amehudumu katika ofisi iliyochaguliwa kwa takriban mwaka mmoja na nusu. Alitambulishwa na mkewe, Usha Vance.

Usha Vance, mke wa mgombea urais anasema: "Tumechaguliwa kusaidia kuongoza nchi yetu kupitia baadhi ya changamoto zake kuu. Ninawashukuru nyote kwa imani mliyoweka kwake.”

Akizungumza Mbele ya umati, wajumbe na wafuasi wa chama, wote walikuwa makini kuona JD Vance ataangazia vipi masuala ya Kigeni ambayo ndiyo kipaumbele ya Marekani.

J.D. Vance, mgombea urais wa chama cha Demokratiki alisema: Kwa pamoja, tutahakikisha washirika wetu wanashiriki katika kutafuta suluhu ya amani duniani, hakuna msaada ya bure tena kwa mataifa ambayo yanasaliti ukarimu wa walipa kodi wa Marekani."

Tetesi kuhusu JD Vance hana uzoefu ulipingwa vikali na baadhi ya wajumbe.

Walter Goodwater, mjumbe wa Texas alisema: "Kweli tunachochagua hapa ni uongozi unaowezekana, na amepata uongozi uliothibitishwa, na yeye ni kijana sio kama sisi wazee.”

Mwanawe Trump Donald Trump Jr, aliwahimiza wamarekani kupigia chama cha Tepublican kwani kilenga kuleta mabadiliko makubwa .

Mtoto wa Donald Trump: Ni chaguo kati ya wamarekani wanaojivunia na watu wasiopenda Marekani , na mwisho, ni chaguo kati ya Marekani na Marekani kwanza."

Mkutano huu unapokamilika hii leo , chaguo sasa linasia kwa wapiga kura kwa jimbo hili la wisconsin ambalo ni jimbo lenye ushindani mkali iwapo wataipigia kura Republican kwa wingi na pia ilikuwa ni kongamano la kushawishi wa Marekani .

Mwandishi wetu Hubbah Abdi, VOA Wisconsin, Marekani.

Forum

XS
SM
MD
LG