Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 01, 2024 Local time: 13:35

Mdahalo wa CNN wa wagombea urais watoa fursa mpya kwa Biden na Trump

Rais wa Marekani Joe Biden na Rais wa zamani wa Marekani na mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Republikan Donald Trump wakishiriki katika mdahalo wa CNN wa wagombea urais wa uchaguzi wa mwaka 2024 katika studio za Kituo cha Televisheni cha CNN huko Atlanta, Georgia, Juni 27, 2024.⁣

Mdahalo huu ni fursa kwa wagombea wote wawili kujaribu kutengeneza tena maelezo ya kisiasa na kuwashawishi wapiga kura waliokuwa hawajaamua nani wampigie kura.⁣
Biden, Mdemokrat aliyeko madarakani, ana fursa ya kuwahakikishia tena wapiga kura kuwa, katika umri wake wa miaka 81, ana uwezo wa kuiongoza Marekani kukabiliana na changamoto mbali mbali.⁣
Wakati huohuo, Trump mwenye umri wa miaka 78 anaweza kutumia fursa hiyo kujaribu kuonyesha kukutwa na hatia ya uhalifu New York hakumshughulishi na kuwashawishi mamilioni ya watu kuwa anasifa za kuweza kurejea tena Ikulu kuongoza nchi.⁣
Mdahalo wa Alhamisi huko Atlanta utaweka rekodi kwa kuongoza kwa mara ya kwanza – haikuwahi kutokea huko nyuma wagombea wawili wanao wania kuingia White House wakikabiliana katika umri mkubwa, na kabla ya hapo CNN haijawahi kuwa wenyeji wa mdahalo wa uchaguzi mkuu wa rais.⁣
https://www.cnn.com/⁣
#debate #presidentialdebate #2024election #biden #trump #reels #videography #voa


Makundi

XS
SM
MD
LG