Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 10:02

Trump na Biden waeleza azma zao kwa wapiga kura kwa nini wanafaa kupigiwa kura


Wagombea urais Marekani 2024 Donald Trump na Joe Biden wakiwa katika mdahalo wa CNN huko Atlanta, Georgia 06.27.2024.
Wagombea urais Marekani 2024 Donald Trump na Joe Biden wakiwa katika mdahalo wa CNN huko Atlanta, Georgia 06.27.2024.

Wagombea urais wa Marekani Joe Biden na Donald Trump walikuwa na mdahalo  wa CNN wa wagombea urais wa kwanza katika mzunguko huu wa uchaguzi jana Alhamisi. 

Joe Biden na Donald Trump kila mmoja alielezea azma yake kwa wapiga kura kwanini anafaa kuwa rais ajaye wa Marekani.

Katika mikutano ya kampeni, Trump anasema uchumi wa Marekani umeharibika.

Katika mdahalo uliofanyika Atlanta ambao uliendeshwa na kituo cha televisheni cha CNN, Trump alisema Marekani nakariri, “ni taifa lililoshindwa kabisa.”

Amesema Biden “amefanya kazi mbaya. Mfumuko wa bei unaiua nchi yetu. Kwa hakika anatuua sisi.”

Rais wa Marekani Joe Biden na Rais wa zamani Donald Trump wakiwa katika mdahalo wa CNN.
Rais wa Marekani Joe Biden na Rais wa zamani Donald Trump wakiwa katika mdahalo wa CNN.

Katika mikutano ya kampeni, Biden anasema amebadili uchumi wa maskini ambao aliurithi kutoka kwa Trump.

Katika mdahalo wa Atlanta, Biden amesema kuna mengi ya kufanywa kuhusu uchumi.

Biden amesema utawala wake “unafanya kazi kushusha bei kwa bidhaa za vyakula, na hicho ndicho watakacho kifanikisha.”

Ukusanayji maoni ya umma unaonyesha hiki kinyang’anyiro cha karibu, huku uchumi na uhamiaji yakiwa masuala ya juu kwa wapiga kura.

Katika mdahalo, Trump anasema Biden ameshindwa kuwalinda Wamarekani kutoka kwa wahamiaji haramu, “ambao wanachukua nafasi za kazi”.

Trump amesema Marekani ina “mpaka ambao ni hatari sana kuliko sehemu nyingine yoyote duniani, ikifikiriwa ni sehemu hatari sana kuliko popote katika duniani, na aliifungua, na hawa wauaji wanakuja katika nchi yetu, na wanawabaka na kuwaua wanawake.”

Katika mdahalo, Biden aliwakumbusha wapiga kura kuhusu utawala wa Trump ulivyozitenga familia kwa sera yake kwa wahamiaji.

Biden amesema wakati Trump alipokuwa rais, “aliwatenganisha watoto na mama zao, na kuwaweka kwenye vichumba vidogo, kuhakikisha kuwa wametengwa na familia zao.”

Kuhusu vita vya Ukraine, Trump amesema Rais wa Russia Vladimir Putin asingeivamia Ukraine kama yeye angekuwa rais.

Vladimir Putin (kushoto) na Volodymyr Zelenskyy
Vladimir Putin (kushoto) na Volodymyr Zelenskyy

Trump amesema kama rais mteule “atahakikisha kuwa vita hivyo vinasuluhishwa kati ya Putin na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy. Kabla ya kuapishwa Januari 20, nitakuwa nimesuluhisha vita hivyo.”

Biden amesema Trump kutokuwa na uungaji mkono na washirika wa Marekani kumeiimarisha Russia na kutishia vita vipana huko Ulaya.

Biden amesema Putin “anaitaka Ukraine yote. Ndicho anachokitaka. Halafu unadhani atasimama hapo tu? Unadhani ataacha, kama akiichukua Ukraine” Undhani nini kitatokea kwa Poland, Belarus?”

Huu ulikuwa na mdahalo wa mapema saia wa urais katika historia ya Marekani, si Trump wala Biden aliyeteuliwa rasmi kutwa mgombea wa chama. Wana siku 75 kuwashawishi wapiga kura kuwachagua kabla ya mdahalo mwingine mwezi Septemba.

Forum

XS
SM
MD
LG