Lakini maneno ya wagombea kuhusu masuala nyetu kama vile uhamiaji na rais wa zamani Donald Trump kukutwa na hatia ya kutoa fedha ili kzuia habari zake zisitangazwe tayari yametawala kila mahali.
Wamarekani lazima wasubiri mpaka Alhamisi kufahamu kama hatia ya uhalifu aliyokutwa nayo Donald Trump itatumika kwenye jukwaa la mdahalo na mpinzani wake Mdemocrat anayewania kuchaguliwa, Rais Joe Biden.
Mwenyekiti Mwenza wa Kampeni ya Biden-Harris
Mitch Landrieu, Mwenyekiti Mwenza Kampeni ya Biden-Harris anasema: “Lakini pia siyo tu kumuita Donald Trump na mhalifu, kama itahusu tabira yake, na mwenendo wake. Kumbuka, kwa hakika mara sita amewahi kuwasilisha suala la kulifisika. Hiyo ina maana kwamba siyo tu mfanyabishara mbaya. Ina maana amewafanyia vibaya watu waliokuwa chini yake ambao kwa hakika walimtegemea yeye kimaisha.”
Trump amekanusha shutuma hizo. Pia ameapa kukata rufaa kwa hatia aliyokutwa nayo.
Wakati Biden amekuwa kwa faragha akijitayarisha kwa mdahalo ujao wa urais...
Trumpa ameamua kuendelea na kampeni zake mwishoni mwa wiki. Alionekana huko Washington…….
…na Philadelphia. Hakuficha azma yake kubwa ya kushiriki mdahalo…
…na kuna nyakati amewauliza wafuasi wake maoni yao kuhusu awe vipi wakati atakapokabiliana na Biden.
Mgombea Urais wa Republikan
Donald Trump, Mgombea Urais wa Republican anasema: “Je niwe mkali na mbaya na kusema kuwa wewe ni rais mbaya katika historia au niwe mzuri na mtulivu na kumuacha azungumze? Au iwe hamsini kwa hamsini? Niwe mgumu.”
Mgombea urais mtarajiwa wa Republican pia alitumia mkutano wa Jumamosi ………..
kuwakumbusha wapiga kura kuhusu msimamo wake kwa wahamiaji wasio na nyaraka halali.
Donald Trump, Mgombea Urais wa Republican anasema: “Siku ya kwanza, tutaanza na hatua kubwa ndani ya nchi kuwafukuza wahamiaji katika historia ya Marekani. Hatuna chaguo.”
Mchakato wa Baadhi ya Vizuizi
Biden hivi karibuni alipitisha mchakato wa baadhi ya vizuizi kwa hifadhi katika mpaka wa kusini.
Lakini pia alizindua hatua wiki iliyopita ambayo itafungua njia kwa uraia kwa wenza wasiokuwa na nyaraka halali ambao wana ndoa na raia wa Marekani. Wakati alipokuwa kwenye ktuo cha televisheni cha NBC, mwenyekiti mwenza wa kampeni ya Biden kuchaguliwa tena alimlaumu Trump na Warepublican kwa hali ilivyo.
Mitch Landrieu, Mwenyekiti Mwenza Kampeni ya Biden-Harris anaeleza: “Mpaka una matatizo. Imekuwa ni kwa miaka 20 mpaka 30 iliyopita katika nchi hii. Joe Biden katika siku ya kwanza, aliwasilisha pendekezo la kina Bungeni kuhusu mageuzi ya uhamiaji. Hawakufanya chochote.”
Mbali ya uhamiaji, inatarajiwa kwamba………. Biden na Trump wataulizwa maswali…… Kuhusu masuala kadhaa mengine …… katika mdahalo wa kwanza wa urais ambapo kituo cha televisheni cha CNN ndiyo itauendesha hapo Juni 27.
Forum