Rais mteule Donald Trump Jumanne ametangaza mipango ya kuunda idara mpya inayoitwa “ Idara ya mapato ya nje” kukusanya ushuru na mapato mengine kutoka mataifa ya kigeni.
Watu 100 ambao walikuwa wakichimba madini kinyume cha sheria katika mgodi wa dhahabu usiofanya kazi nchini Afrika Kusini walifariki baada ya kunaswa chini ya mgodi huo kwa miezi kadhaa, huku polisi wakijaribu kuwaondoa huko, kundi linalowakilisha wachimba migodi hao lilisema Jumatatu.
Chama tawala nchini Chad kimepata viti vingi katika uchaguzi wa bunge wa mwezi Disemba, ambao ulisusiwa na vyama vikuu vya upinzani ambapo wachambuzi wanasema utaimarisha nguvu za kisiasa za rais, matokeo ya awali yameonyesha.
Jaji wa Mahakama ya New York amemhukumu Donald Trump kuachiliwa bila ya masharti yoyote leo Ijumaa kwa kuficha malipo ya pesa kwa mcheza filamu za ngono licha ya juhudi za rais-mteule wa Marekani kufanya juhudi za dakika za mwisho kuepuka kuwa mhalifu wa kwanza katika White House.
Congo Alhamisi imeipiga marufuku mtandao wa habari wa Al Jazeera kutokana na kutanganza mahojiano yake na kiongozi wa kundi la uasi ambalo limekamata eneo la mashariki mwa nchi katika siku za karibuni.
Serikali ya kijeshi ya Myanmar imewaachia huru zaidi ya wafungwa 6,000 na kupunguza adhabu za vifungo vya wafungwa wengine, kama sehemu ya msamaha kwa watu wengi katika kuadhimisha miaka 77 ya uhuru wake kutoka kwa Uingereza siku ya Jumamosi.
Watu kumi waliuawa na 35 kujeruhiwa baada ya mshukiwa kuvurumisha gari lake kwenye umati wa watembea kwa miguu katika Barabara yenye shughuli nyingi ya French Quarter huko New Orleans leo saa tisa na robo alfajiri siku ya Jumatano kwenye mtaa wa Bourbon.
Mamlaka za Ujerumani zilipokea taarifa za tahadhari mwaka jana kuhusu mshukiwa wa shambulizi la gari kwenye soko la Christmas, ofisi ya serikali imesema Jumapili, huku maelezo zaidi yakitolewa kuhusu watu watano waliouawa katika shambulizi hilo.
Mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza usiku kucha hadi Jumapili yameua watu 20 wakiwemo watoto watano, maafisa wa idara za matibabu za Palestina wamesema.
Wajerumani Jumamosi wameomboleza waathirika wa shambulizi lililofanywa na daktari raia wa Saudi Arabia ambaye aliendesha kwa makusudi gari lake ndani ya umati wa watu na kuwagonga wale waliokuwa kwenye soko la kuuza bidhaa za siku kuu ya Christmas, na kuua watu watano.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, Alhamisi ameziomba nchi tajiri kutimiza ahadi zao ya kuzisaidia nchi masikini katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Polisi nchini Korea Kusini wamesema wamepeleka maafisa kufanya upekuzi katika ofisi ya rais Yoon Suk Yeol leo Jumatano, kama sehemu ya uchunguzi unaoendelea baada ya kutangaza matumizi ya sheria ya kijeshi.
Mahakama ya Katiba ya Zambia Jumanne kwa kauli moja imetoa maamuzi kuwa rais wa zamani Edgar Lungu hawezi kuwania kugombea kwenye uchaguzi wa 2026 kwa kuwa tayari amehudumu mihula miwili.
Mgombea wa chama tawala nchini Ghana cha New Patriotic, Makamu wa Rais Mahamudu Bawumia Jumapili amekubali kushindwa katika uchaguzi wa rais baada ya kushindwa kushughulikia kero kubwa ya wananchi kutokana na hali mbaya ya uchumi.
Vituo vya kupigia kura katika uchaguzi wa rais na bunge nchini Ghana vimefunguliwa Jumamosi, katika uchaguzi ambao ni mtihani kwa taifa hilo la kidemokrasia ambalo lilitikiswa na machafuko mabaya na mapinduzi ya kijeshi katika miaka ya nyuma.
Iran ilisema Ijumaa imefanya zoezi la mafanikio la kurusha chombo cha anga za juu, kwa ajili ya programu yake mpya ambayo nchi za Magharibi zinadai inaboresha programu ya Tehran ya makombora ya balistiki.
Waziri Mkuu wa Ufaransa Michael Barnier amewasilisha barua ya kujiuzulu kwake asubuhi ya leo katika makazi ya rais ya Elysee.
Rais wa Marekani Joe Biden amerejea nchini mapema leo akitua katika uwanja wa Andres Airforce Base katika jimbo la Maryland akitoeka nchini Angola.
Baada ya miezi minne, pamoja na kufukuzwa kwa ujumbe wa serikali, mazungumzo ya amani ya Sudan Kusini yaliyokwama yameanza tena Jumatano nchini Kenya, ikiwa juhudi ya karibuni zaidi ya kumaliza ghasia ambazo zimevuruga kabisa uchumi na uthabiti wa taifa hilo changa.
Shirika la Mpango wa Chakula Duniani WFP linaeleza hali ya ukataji tamaa unaongezeka Gaza kutokana na baa la njaa linaloongezeka.
Pandisha zaidi