Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:25

Wachimba migodi haramu 100 wafariki katika mgodi wa madini nchini Afrika Kusini


Watu wafuatilia ukaguzi ukifanywa na waziri wa polisi wa Afrika Kusini kwenye mgodi ambapo mamia ya wachimba migodi haramu wanaaminika kujificha chini ya ardhi, Novemba 15, 2024. Picha ya Reuters
Watu wafuatilia ukaguzi ukifanywa na waziri wa polisi wa Afrika Kusini kwenye mgodi ambapo mamia ya wachimba migodi haramu wanaaminika kujificha chini ya ardhi, Novemba 15, 2024. Picha ya Reuters

Watu 100 ambao walikuwa wakichimba madini kinyume cha sheria katika mgodi wa dhahabu usiofanya kazi nchini Afrika Kusini walifariki baada ya kunaswa chini ya mgodi huo kwa miezi kadhaa, huku polisi wakijaribu kuwaondoa huko, kundi linalowakilisha wachimba migodi hao lilisema Jumatatu.

Sabelo Mnguni, msemaji wa jamii zilizoathiriwa na uchimbaji madini aliliambia shirika la habari la Associated Press kwamba simu ya mkononi iliyotumwa juu ya mgodi huo na baadhi ya wachimba migodi waliookolewa siku ya Ijumaa, ilikuwa na video mbili zikionyesha miili kadhaa iliyofunikwa kwa plastiki chini ya ardhi.

Mnguni alisema “takriban watu 100 walifariki katika mgodi katika mkoa wa kaskazini magharibi ambako polisi walianzisha operesheni mwezi Novemba kuwalazimisha wachimba migodi kuondoka.

Wanashuku watu hao walikufa kwa njaa au kwa sababu ya kukosa maji mwilini, Mnguni alisema.

Alisema miili 18 iliondolewa ndani ya mgodi huo tangu Ijumaa.

Msemaji wa polisi Brigedia Sebata Mokgwabone alisema bado wanachunguza taarifa kujua ni miili mingapi iliyopatikana na ni manusura wa ngapi waliookolewa baada ya operesheni ya uokoaji kuanzishwa Jumatatu.

Forum

XS
SM
MD
LG