Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 18, 2025 Local time: 09:48

Trump atangaza mipango ya kuunda idara mpya ya mapato ya nje


Rais mteule Donald Trump akizungumza wakati wa mkutano na magavana kutoka chama cha Republican, kwenye makazi yake ya Mar-a-Lago Florida, Januari 9, 2025. Picha ya AP
Rais mteule Donald Trump akizungumza wakati wa mkutano na magavana kutoka chama cha Republican, kwenye makazi yake ya Mar-a-Lago Florida, Januari 9, 2025. Picha ya AP

Rais mteule Donald Trump Jumanne ametangaza mipango ya kuunda idara mpya inayoitwa “ Idara ya mapato ya nje” kukusanya ushuru na mapato mengine kutoka mataifa ya kigeni.

“Tutaanza kuwatoza wale wanaopata pesa kutoka kwetu kupitia biashara, wataanza kulipa,” Trump alisema kwenye mtandao wake wa kijamii, Truth Social.

Alilinganisha mpango wake wa kuunda idara hiyo na Idara ya kukusanya mapato ya ndani, ambayo ni mamlaka ya kitaifa ya kukusanya kodi ya ndani.

Kuunda idara hiyo mpya kutahitaji sheria itakayopitishwa na bunge, na Warepublican wana wingi wa viti katika Baraza la Wawakilishi na katika Baraza la Seneti.

Forum

XS
SM
MD
LG