Mkurugenzi Mtendaji huyo wa Tesla alikuwa muhimu katika kuchaguliwa tena kwa Trump kwa mchango wake wa zaidi ya robo ya dola bilioni kwenye kampeni ya Trump kwa mujibu wa jarida la Forbes. Musk anatarajiwa kuwa mkuu wa Idara mpya ya Trump.
Ufanisi wa Serikali, pamoja na Vivek Ramaswamy, mjasiriamali wa kampuni ya masuala ya biolojia.
Ripoti zinaeleza kuwa Musk anatazamiwa kuketi kwenye sherehe za kuapishwa huko pamoja na mabilionea wenzake Mkurugenzi Mtendaji wa Amazon Jeff Bezos na Mkurugenzi Mtendaji wa Meta Mark Zuckerberg.
Ingawa sio kawaida kuwaalika viongozi wa kigeni, Trump amewaalika kadhaa.
Trump pia amemwalika Rais wa China Xi Jinping ambaye anatuma mjumbe. Waziri Mkuu wa Italia mwenye mrengo mkali wa kulia Giorgia Meloni pia amepokea mwaliko, lakini amesema hana uhakika kama ratiba yake itamruhusu kuhudhuria.
Forum