Amesema kwamba hilo litatokea iwapo msaada wa Marekani utasitishwa , na kwamba mamilioni ya watu huenda wakafa wakati makali ya ugonjwa huo yakiongezeka. Wakati wa mahojiano na shirila la habari la AP, Winnie Byanyima aliesema kuwa maambukizi ya HIV yamekua yakishuka katika miaka ya karibuni, wakati kukiwa na maambukizi mapya milioni 1.3 pekee yaliorekodiwa 2023, ikiashiria kushuka kwa asilimia 60 tangu rekodi kubwa ya maambukizi ya 1995.
Hata hivyo tangu tangazo la rais wa Marekani Donald Trump kwamba Marekani ingesitisha msaada wa kigeni kwa siku 90, Byanyima alisema kuwa maafisa wanakadiria kwamba kufikia 2029, huenda kukawa na maambukizi mapya milioni 8.7, ongezeko la vifo mara 10 hadi watu milioni 6.3, ikiwa na maana ya ongezeko la mayatima milioni 3.4.
Akizungumza akiwa Uganda, Byanyima aliomba serikali ya Marekani isisitishe msaada wake ghafla kwa kuwa hatua hiyo imezua hofu na wasiwasi miongoni mwa mataifa mengi ya kiafrika, yaliyoathiriwa zaidi na Ukimwi. Alitoa mfano wa Kenya ambapo wafanyakazi 500 wa HIV walisimamishwa kazi mara moja huku maelfu wengine nchini Ethiopia wakichukuliwa hatua sawa na hiyo, hali iliyoacha maafisa wa afya bila uwezo wa kufuatilia maambukizi.
Karibu dola milioni 400 za kimarekani hupelekwa Uganda, Msumbiji na Tanzania kila mwaka, Byanyima alisema. Aliongeza kuwa kufikia sasa hakuna mataifa mengine yaliyojitokeza kuziba mwanya utakaoachwa na usitishwaji wa msaada wa Marekani.
Forum