Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 18, 2025 Local time: 09:42

Jaji wa Mahakama ya New York amhukumu Trump kuachiliwa bila masharti


Kesi ya Rais-mteule Donald Trump yasikilizwa katika mahakama ya New York.
Kesi ya Rais-mteule Donald Trump yasikilizwa katika mahakama ya New York.

Jaji wa Mahakama ya New York amemhukumu Donald Trump kuachiliwa bila ya masharti yoyote leo Ijumaa kwa kuficha malipo ya pesa kwa mcheza filamu za ngono licha ya juhudi za rais-mteule wa Marekani kufanya juhudi za dakika za mwisho kuepuka kuwa mhalifu wa kwanza katika White House.

Mahakama hii imefanya maamuzi halali yanayoruhusu kuingizwa katika hukumu kwa mtu aliyekutwa nah ai bil ya kuingilia ofisi ya juu zaidi katika nchi, ni kuachiliwa bila ya masharti,” alisema jaji wa New York Juan Merchan alipokuwa akisoma hukumu mahakamani ambapo alihudhuria kusikiliza hukumu hiyo kwa njia ya mtandao.

Trump alisema katika hukumu ya Ijumaa kwa kukutwa na hatia ya uhalifu kutokana na kuficha malipo ya pesa kwa mcheza filamu za ngono kuwa kesi hiyo imekuwa mbaya sana kwake.

Utoaji wa hukumu siku chache kabla ya kuapishwa kwake Januari 20, unafunga kesi hiyo ambayo imekuwa ikiangaziwa kwa muda na juhudi zake zilizofanikiwa mwaka jana za kutaka kuingia White House. Jaji Merchan ambaye alisimamia kesi hiyo kwa wiki sita, aliashiria awali hakuwa na mpango wa kufunga jela Trump au kumtoza faini.

Akionekana kwenye video kutoka Florida akiwa na wakili wake Todd Balance, Trump amesema alikuwa hana hatia na hakufanya kosa lolote.
“Sina hatia hata kidogo, sikufanya kosa lolote, alisema Trump ambaye hakutoa ushahidi wake mahakamani wakati wa kesi hiyo ya iliyodumu kwa wiki sita mwaka jana.

Forum

XS
SM
MD
LG