Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 09, 2025 Local time: 12:51

EU yasema haitakubali mashambulizi katika mipaka yake


 Jean-Noel Barrot
Jean-Noel Barrot

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Noel Barrot alisema Jumatano kuwa (Januari 8) Umoja wa Ulaya hautaruhusu mataifa mengine kushambulia mipaka yake huru, kauli ya Waziri huyo inajiri kufuatia maoni ya Rais mteule wa Marekani Donald Trump kuhusu kutwaa eneo la Greenland.

FILE PHOTO: Rais-mteule Donald Trump
FILE PHOTO: Rais-mteule Donald Trump

Trump alikataa Jumatatu (Januari 6) kuelezea kwa undani iwapo atachukua hatua za kijeshi au kiuchumi kama sehemu ya nia yake ya kutaka Marekani kuchukua udhibiti wa Greenland, pamoja na Mfereji wa Panama.

Akizungumza katika shirika la Radio la Inter Milan Jean-Noel Barrot alieleza kuwa haamini kwamba Marekani ingevamia kisiwa kikubwa cha Arctic ambacho kimekuwa sehemu ya Denmark kwa zaidi ya miaka 600.

Maoni ya Trump yalielezea zaidi ajenda ya upanuzi, wiki mbili kabla ya kuapishwa ofisini kwenye haya kuapishwa Januari 20 mjini Washington.

Alipoulizwa kuhusu vikwazo vya Umoja wa Ulaya nchini Syria ambavyo kwa sasa vinazuia utoaji wa misaada ya kibinadamu na kukwamisha nchi hiyo, Barrot alisema vinaweza kuondolewa haraka.

Forum

XS
SM
MD
LG