Waziri Mkuu wa Italial Giorgia Meloni alifanya ziara ya kushtukiza huko Forida kukutana na Donald Trump Jumamosi jioni, kama kiongozi mkuu wa Ulaya kutaka kujenga mahusiano na rais-mteule kabla ya kuapishwa kwake Januari 20.
Watu waliokuwa Mar-a-Lago kwa Trump walimkaribisha Meloni kwa shangwe baada ya rais-mteule kumfahamisha kwa watu, kwa mujibu wa kanda za video kwenye mitandao ya kijamii zilizotumwa na waandishi wa habari na wengine.
Meloni alionekana kama mshirika mwenye nguvu kwa Trump hasa kutokana na yeye kuwa M-conservative na utulivu kwa ushirika wa mrengo wa kulia ambao ameuongoza Italy tangu mwishoni mwa mwaka 2022.
Pia alisukuma mbele uhusiano wa karibu na bilionea Elon Musk, mshirika wa karibu wa Trump ambaye ametumia karibu dola robo bilioni kumsaidia kuchaguliwa tena. “Hii inafurahisha sana. Niko hapa na mwanamke jasiri, waziri mkuu wa Italia,” Trump aliuambia umati uliokuwa Mar-a-Lago, kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari. “Kwa kweli ameichukua Ulaya kwa kishindo.”
Forum