Utawala wa kijeshi wa Mali Jumatano umemkamata mwanasiasa mashuhuri nchini kutokana na kukosoa utawala wa kijeshi wa nchi jirani ya Burkina Faso, mtoto wake wa kiume pamoja na vyanzo vya mahakama wamesema.
Mwanauchumi wa Morocco ambaye anafahamika kutokana na harakati zake za kutetea haki za binadamu amezuiliwa kufuatia matamshi ya kukosoa serikali kupitia mitandao ya kijamii.
Rais wa Kenya Dr. William Ruto amekutana na mkurugenzi wa idara ya ujasusi ya Marekani CIA William Burns katika kikao ambacho kilihudhuriwa na mkuu wa ujasusi wa Kenya Noordin Haji.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameshutumu kabisa mashambulizi dhidi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa, wakati wa mkutano kwa ajili ya Lebanon, leo alhamisi mjini Paris, Ufaransa.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ametangaza msaada wa dola milioni 135 zaidi kwa ajili ya wapalestina wakati wa ziara yake ya mashariki ya kati.
Kenya imeanza kuhamisha ndovu kutoka kwenye mbuga ya kitaifa ya wanyamapori ya Mwea, iliyopo mashariki mwa Nairobi baada ya idadi yao kuongezeka kutoka 50 hadi 150, na kwa hivyo kulemea mbuga hiyo yenye ukubwa wa kilomita 42 mraba.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amekutana na viongozi wa Uingereza na NATO mjini London leo Alhamisi kwa mazungumzo yaliyoangazia mpango wa ushindi dhidi ya Russia.
Mwandishi wa Korea Kusini Han Kang amepewa tuzo ya Nobel katika uandishi wa fasihi kutokana na mashairi yake yanayoangazia uhalisi wa kihistoria na kufichua matatizo ya maisha yanayomkumba binadamu.
Israel Jumapili iliongeza mashambulizi yake ya mabomu kaskazini mwa Gaza na kusini mwa Lebanon katika vita vipana dhidi ya makundi ya wanamgambo yanayoungwa mkono na Iran katika kanda hiyo.
Umati wa watu Jumapili ulishiriki katika maandamano ya kuunga mkono Palestina na Israel na hafla za kumbukumbu zimefanyika kote duniani katika mkesha wa maadhimisho ya kwanza ya mashambulizi ya Hamas dhidi ya Israel.
Mahakama ya Katiba ya Afrika Kusini imesema Alhamisi kuwa mwezi ujao itasikiliza kesi iliowasilishwa na vyama viwili vya upinzani ikilenga kufufua mchakato wa kutokuwa na imani na Rais Cyril Ramaphosa.
Seneta wa Marekani JD Vance, mgombea mwenza wa Donald Trump wa chama cha Republikan, alishindana na Gavana wa Minnesota Tim Walz, ambaye ndiye mgombea mwenza wa Kamala Harris wa chama cha Demokratik katika mdahalo wa televisheni ya kitaifa siku ya Jumanne.
Familia zinazokimbia mzozo unaopamba moto nchini Lebanon ziliingia kwa wingi Jumatano nchini Syria, zikisubiri kwa saa kadhaa katika msongamano wa magari kupata usalama mdogo katika nchi hiyo nyingine inayokumbwa na vita.
Chini ya ulinzi mkali, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy Jumapili alikitembelea kiwanda cha kutengeneza silaha katika jimbo la Pennsylvania.
Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric ametoa wito kwa wanachama wote wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutafuta namna ya kupunguza uhasama kati ya Israel na Lebanon.
Israel leo imeendelea kutekeleza mashambulizi ya kijeshi katika eneo la Ukingo wa Magharibi libalokaliwa kimabavu, ikisema kwamba inalenga kuyavunja kabisa makundi ya wanamgambo na kuzuia ongezeko la mashambulizi dhidi ya wa Israel.
Shambulio la anga la Israel lauwa takribani watu 14 wakiwemo watoto wawili, wakati lilipopiga shule ya Umoja wa Mataifa iliyokuwa hifadhi ya familia za Wapalestina waliopoteza makazi katikati ya Gaza siku ya Jumatato, maafisa wa hospitali wamesema.
Mwanadiplomasia wa ngazi ya juu ameitaka BRICS kuungana wakati ikikabiliwa na fikra za vita baridi
Maafisa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamesema dozi 50,000 za chanjo dhidi ya Mpox kutoka Marekani ziliwasili Jumanne, wiki moja baada ya shehena ya kwanza kutoka Umoja wa Ulaya kuwasili nchini humo.
Iran imekanusha ripoti kwamba sehemu iliyopigwa na makombora nchini Syria, ni ya washirika wake.
Pandisha zaidi