Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:15

Mgombea wa chama tawala nchini Ghana akubali kushindwa katika uchaguzi wa rais


Wafuasi wa chama cha upinzani nchini Ghana wakisherekea ushindi wa mgombea wa chama cha NDC na rais wa zamani John Dramani Mahama, Disemba 7, 2024. Picha ya Reuters
Wafuasi wa chama cha upinzani nchini Ghana wakisherekea ushindi wa mgombea wa chama cha NDC na rais wa zamani John Dramani Mahama, Disemba 7, 2024. Picha ya Reuters

Mgombea wa chama tawala nchini Ghana cha New Patriotic, Makamu wa Rais Mahamudu Bawumia Jumapili amekubali kushindwa katika uchaguzi wa rais baada ya kushindwa kushughulikia kero kubwa ya wananchi kutokana na hali mbaya ya uchumi.

Kushindwa katika uchaguzi wa Jumamosi kunamaanisha kumalizika kwa utawala wa mihula miwili wa chama cha NPP chini ya uongozi wa Rais Nana Akufo-Addo, uliokabiliwa na mzozo mbaya wa uchumi, mfumuko mkali wa bei na kushindwa kulipa madeni.

“Wananchi wa Ghana wamezungumza, wananchi wamepiga kura ya mabadiliko kwa wakati huu na tunayaheshimu kwa unyenyekevu,” Bawumia alisema katika mkutano na waandishi wa habari. Alisema amempigia simu mpinzani wake mgombea wa Chama cha National Democratic Congress (NDC) na rais wa zamani John Mahama, kumpongeza.

Mahama amethibitisha kwenye mtandao wa X kwamba alipokea simu ya pongezi kutoka kwa Bawumia kutokana na “ushindi wake mkubwa.”

Forum

XS
SM
MD
LG