Mamlaka za Israel wakati huo huo, wamemuruhusu Kardinali Pierbattista Pizzaballa, kiongozi wa kanisa katoliki katika eneo takatifu kuingia Gaza na kuongoza misa ya kabla ya Christmas na waumini wa jamii ndogo ya Wakristo katika eneo hilo.
Shambulizi kwenye jengo la shule linalohifadhi wasiokuwa na makazi huko Gaza City liliua watu wanane, wakiwemo watoto watatu, kulingana na wizara ya afya ya Gaza.
Jeshi la Israel limesema lilifanya shambulizi la uhakika kuwalenga wanamgambo wa Hamas waliokuwa wamejificha huko.
Forum