Kwa mujibu wa shirika la habari AP, mahakama hiyo imeamua kuwa muda ambao Lungu alihudumu kama rais wa taifa hilo la kusini mwa Afrika kati ya 2015 na 2016 kufuatia kifo cha Michael Sata akiwa ofisini kinahesabiwa kama muhula kamili.
Lungu alishinda uchaguzi kwa muhula wa pili kuanzia 2016 hadi 2021. Mwaka uliopita, alitangaza kujitosa tena kwenye ulingo wa siasa akilenga kugombea dhidi ya rais wa sasa Hakainde Hichilema, kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Kesi hiyo imekuwa ikifuatiliwa na watu wengi nchini Zambia kiasi kwamba uamuzi wa jopo la majaji saba ulitangazwa moja kwa moja kwenye televisheni na radio za taifa.Lungu alishindwa na Hichilema katika wa 2021, na uamuzi wa Jumanne una maana kwamba hataweza kushiriki kwenye uchaguzi huo.
Kesi hiyo hata hivyo imegubikwa na shutuma kadhaa kuhusu uingiliaji kati wa kisheria baada ya Hichilema kuwafukuza kazi majaji watatu kutoka katika mahakama ambayo ilifanya maamuzi kumpendelea Lungu katika kesi ya awali inayohusishwa na uchaguzi wa 2016.
Forum